MAOMBI YA KUHAMASISHA AMANI KATIKA TAIFA LA TANZANIA
Suala la amani na usalama ndani ya nchi ama taifa ni
jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa unadumu sanjari na kumwomba Mungu juu
ya jambo hilo.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es saalam na askofu
Daktari Mgulu kilimba wa huduma ya christian mission Fellowship wakati wa ibada
maalum yamaombi ya kuhamasisha amani nchini.
Aidha askofu DK Kilimba alisema neno la
Mungu limetuagiza katika 1timotheo 2:1-2; kuwa kabla ya mambo yote nataka dua,
sala, maombezi na shukurani vifanyike kwa watu wote; kwaajili ya Wafalme na
wenye mamlaka, tuishi kwa utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu ,tukiwa
Kanisa la Mungu, tumechukua hatua hii ya kuanza kuliombea Taifa kwa kuugua mno
ili Amani tuliyopewa na Mungu na
kuenziwa na waasisi wa Taifa hili iweze kudumishwa.
"ndugu zangu watanzania sote tufahamu
kuwa, msimamo tuliyojiwekea katika katiba yetu ya jamhuri ya muungano wa tanzania, ni
kupiga marufuku kila namna ya ubaguzi ukiwemo wa kijinsia, rangi na kidini.
Katiba ya 1977 ibara 13(5) ambapo kwa upande wa madhehebu ya dini tanzania tuna
dini kubwa tatu na nyingine ndogondogo dini kubwa ni ukristo, uislamu na dini
za kijadi.toka mwanzo wakristo na waislamu tumekuwa tukishirikiana pamoja
katika misiba, sherehe mbalimbali, kuoleana, kuishi katika nyumba moja na kufanya shughuli za kijamii kwa pamoja
bila kubaguana kabla na baada ya miaka
hamsini ya uhuru nchi yetu" alisema askofu dk kilimba .
Aliongeza kuwa wakristo na watanzania kwa
ujumla ni vyema kufahamu kuwa, hakuna nchi
yeyote katika bara la afrika
yenye idadi kubwa ya wakristo na waislamu wanaoishi kwa amani na upendo kama tanzania,ila kwa sasa watu wasioitakia
amani nchi yetu wanataka kupenyeza chuki za kidini ili isiwe nchi ya amani bali ya vurugu.
Kutokana na hayo hivi karibuni tumeshuhudia
kuwepo kwa vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa kidini kwa baadhi ya vikundi toka
makundi ya dini kubwa kudai haki zao ambazo kimsingi wanaona wanastahili kuwa
nazo sawa na dini nyingine, hali hii imefanya vikundi hivi vitumie vyombo vya
habari hususani redio, magazeti na machapisho mbalimbali kueleza hisia zao kwa
jamii, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa mgawanyiko katika jamii iliyokuwa
imeshikamana na mgawanyiko huu unazidi kukua siku hadi siku na kusababisha hali
ya chuki kwa mamlaka ya nchi na hatimaye dini moja na nyingine.
"Baada ya kufanya utafiti wa kina
kwanini kuwepo na chuki baina ya makundi ya dini na serikali tumeona kuwa,
makundi haya ya dini yanaiona serikali inawanyima haki zao na inapendelea dini moja na hivyo kutumia mfumo wake katika
utawala, ambapo madai ya kundi hilo
yanawapelekea kuwafanyia vurugu waumini wa kundi wanalosadiki kuwa
linapendelewa na serikali, jambo ambalo linawafanya wanaofanyiwa vurugu
wasitumie uhuru wao wakufanya ibada
ambayo kimsingi walipewa mungu na kuandikwa katika katiba ya nchi yetu",
aliongeza.
Pamoja na hayo tukiwa kanisa la mungu, hali hii
inatupelekea kuona kuwa bado serikali yetu haijawajibika ipasavyo katika
kuelekeza sera na shughuli zake kwa lengo la kuhakikisha kuwa sheria za nchi
zinalindwa na kutekelezwa, kimsingi haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya
umma vinapaswa kutoathiriwa kabisa na
matumizi mabaya ya uhuru wa haki za watu binafsi.
Hivyo askofu Dk Kilimba aliongeza kusema kanisa baada
ya kumlilia mungu kwa machozi na maombi mengi, tumeamua kuchukua mwelekeo wa
uwajibikaji usio wa maneno tu, kwani
suala la kutoa matamko ya kulaani
limefanywa na dini na serikali kwa mkazo mkubwa. Na kwa upande wa
serikali, watawala wa nchi yetu wamekuwa
wakilaani na kukemea, ubaguzi wa dini,
rushwa na ufisadi katika taifa hili bila mafanikio na hata leo tunawaona
vijana wanatwangana hadharani kutokana na kushamili kwa rushwa ,hii yote ni kwa
sababu hayo ni vita ya kiroho na
inapaswa kukemewa na viongozi wa dini na watawala wanapaswa kuchukua hatua. Kwa
jinsi hii, kanisa limelitazama jambo hili kiroho zaidi kwa kutambua kuwa chuki
na rushwa ni roho kamili inayotoka kwa shetani, hivyo watu wa kiroho tunalo
jukumu la kuzipinga hila zote za shetani kwa dua,
sala na maombi ili kuleta amani ya kudumu katika taifa letu, ambalo linasifika
kuwa ndiyo kitovu cha amani afrika na duniani.
Akielezea kwa hisia alisema "Ndugu zangu wakristo
na viongozi wa dini, ikumbukwe na
izingatiwe kuwa nyumba za ibada ni
sehemu ya kumwabudu mungu, hivyo
zitumike kuhubiri dini tuliyo amuriwa na mungu na sio siasa, na pasiwe mahali
pa kuandaa na kuchochea vurugu na chuki miongoni mwetu kwani viongozi wa
dini wanaaminiwa sana na waumini wao
na lolote watakalo waambia waumini,
huaminiwa kuwa limetoka kwa mungu".
Aidha aliongeza kuwa ikumbuke kuwa, tunafanya kila kitu
vizuri zikiwemo ibada zetu kwasababu ya amani tuliyonayo, amani isipokuwepo
hakuna kitu kinaweza kufanyika katika nchi iwe kwa waumini na wasio wauimini,
iwe kwa maskini au matajiri. Amani ikishaondoka, matajiri au wenye pesa
watakimbia na kuwa wakimbizi wa nchi zingine, huku masikini wakikosa mahali pa
kwenda na kuishia kuuawa na kupoteza maisha. Kwa hiyo ni vema kuitunza amani
yetu na kuilinda,kamwe tusiichezee amani tuliyonayo katika nchi yetu, hii ni
tunu tuliyopewa na mungu na kuachiwa na waasisi wa nchi yetu ili tuienzi, hivyo
kila mmoja wetu ni mdau wa amani. Mkulima anahitaji amani ili aweze kupata
mazao shambani mwake; daktari anahitataji amani ili afanye kazi zake vema
hospitalini, kadhalika mfanya biashara na mwanasiasa wote wanahitahi amani.
Pamoja na hayo yote askofu Dk Kilimba alisema kuwa kamanda
Suleiman Kova wa kanda maalum ya dar es saalamkwa ameonesha juhudi zake za kuifanya Dar-es-saalam iendelee kuwa
bandari ya amani, ameonesha ushupavu na umadhubuti mkubwa katika kauli zake,
kwani mchango wake umeleta heshima iliyotukuka katika vyombo vya dola
nchini na kwa watanzania wote.
Katika maombi hayo ya kuhamasisha amani nchini yalitanguliwa
na maombi ya watu 12 waliowakilisha zaidi makabila 120 ya tanzania kwa kutumia lugha za makabila hayo kama
alama ya umoja na mshikamano.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni