YESU NI JIBU

Jumapili, 1 Februari 2015

WATU WATATU WAPOTEZA MAISHA MARA BAADA YA PIKIPIKI WALIOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGANA USO KWA USO LA LORI NA KUWAKA MOTO MKOANI IRINGA:

Lori  aina  ya  fuso  likiwa  limeharibika  kupita  kiasi baada ya  kugongana na boda  boda  eneo la  Kihesa  Kilolo mjini Iringa usiku  huu na kusababisha   vifo vya  watu  watatu  waliokuwa  wamepakizana katika  boda  boda  hiyo.
Hivi ndivyo  lori   lilivyoharibika baada ya kugongana na pikipiki,
Wananchi  wakishuhudia  ajali  hiyo  ya  Lori na boda  boda. 
Hii  ndio  pikipiki  iliyoteketea  kwa moto baada ya ajali.
Hili  ndilo  eneo ambalo miili ya  vijana  hao  watatu  iliteketea kwa moto baada ya ajali.
Picha kwa hisani ya matukio blog.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni