Kiongozi ni mtu mwadilifu ,mwenye imani,asiyelaumiwa kwa jambo
lolote baya sanjari na kuwa na imani ya kuwatumikia jamii inayomzungukwa kwa
lengo la kuwaleta maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na askofu wa
jimbo la Mashariki kaskazini askofu Geofrey Massawe katika hafla ya kuwasimika
na kuwaweka wakfu viongozi wa sehemu mbalimbali katika jimbo hilo ambapo
amesema kuwa sifa ya kiongozi ni kuwatumikia waumini na jamii inayomzunguka.
Askofu Geofrey Masawe akiwaweka wakfu viongozi mbalimbali katika jimbo la mashariki kaskazini.
Kutoka kushoto ni katibu wa jimbo la mashariki kaskazini Charles Shilla na katikati niaskofu jimbo hilo Askofu Geofrey Masawe na kulia ni makamu askofu.
Aidha Askofu Massawe amesema kuwa ni vyema kiongozi
anapochaguliwa ama kuteuliwa ni vizuri kuwatumikia wananchi na sio kutekeleeza
matakwa yake binafsi jambo ambalo limesababisha mianya mbalimbali ya rushwa na
kushindwa kuleta maendeleo.
''Ili kutokomeza tatizo la rushwa na kushindwa kutekeleza
majukumu ya kila siku kiongozi anatakiwa kuwa jasiri na mwadilifu katika
majukumu yake ya kila siku kama kiongozi ambaye ni kioo cha jamii'',alisema
askofu Masawe.
Hata hivyo amewataka viongozi na wananchi kwa ujumla
kusimamia, kulinda na kutunza amani ambayo imeasisiwa na waasisi wa taifa hili
kabla ya uhuru mpaka sasa kwa kusudi la kudumisha amani na usalama ndani ya
taifa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Amani na Utulivu iliopo nchini ni wajibu wa kila
mtanzania kuendelea kulinda na kudumisha maana katika kipindi hiki cha uchaguzi
na kuwasihi viongozi mbalimbali kuwa makini na kuwa makini na waadilifu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni