1.Rafiki
ni nani ?
answer:ni mtu ambaye unaweza kumwamini ,kujiweka
wazi kwake.
ni mtu anayeweza kuchangia
kufaulu na ustawi wako katika maisha.
2.Mfalme
yupi ambaye amezikwa katika makaburi ambayo amejichimbia katika mji wa Daudi na
alikufa katika mwaka wa ngapi wa utawala wake.
Answer: Ni mfalme Asa
aambaye alikufa katika mwaka wa 41 wa kumiliki kwake
2nyakati 16:13-14
3.Neno kuabudu lina maana gani?
Answer:Ni
tendo linalogusa akili,hisia,nafsi na utu wa mtu na mwili pia kwa
kusujudu,kuanguka kifudifudi,au uso kwa uso
mwanzo
17:3 Tendo hilo hufanywa pasipo ushawishi wa kitu ,wala si nje ya moyo wa
kumtambua Mungu kuwa wa thamani kuliko
kitu chochote anayestahili kupewa ibada ya pekee na kupelekea kujitoa kwake
bila unafki wala ubinafsi .
4.Karama Tisa za Roho Mtakatifu
zimegawanyika katika mafungu matatu nazo ni zipi
1.Karama za ufunuo
· Neno la maarifa
· Neno la hekima
· kupambanua Roho
2.Karama
za uwezo
· imani
· karama za kuponya
· matendo ya miujiza
3.Karama
za usemi
· Unabii
· Aina za lugha
· Tafsiri za lugha
5.Daudi
na Jonathani walikuwa marafiki ni kitu (siri)gani kilichosababisha urafiki wao
udumu toa sababu sababu nne ama siri nne.
1. mwambatano ulianzia katika roho zao.
2. upendo wa kweli kati yao(1sam 18:1)
3. utayari wa kila mmojaa wao kuwa mwaminifu
katika patano la urafiki wao(1sam18:3)
4. upendo wenye msukumo wa kutoa na kujitoa kwa
hiari kila mtu kwa mwenzie(1sam18:4)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni