YESU NI JIBU

Jumamosi, 14 Februari 2015

KAULI YA KIONGOZI WA KANISA KATOLIKI DUNIANI:



Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amesema kuwa wanandoa wasio na watoto ni chanzo cha kizazi cha ulafi.
Akizungumza mbele ya umati mkubwa katika bustani ya St. Peters,papa Francis aliendelea kusema kuwa ni jamii yenye uzuni ambayo inaweza kufikiri kwamba watoto ni mzigo ama hata ni hatari.
Kufuatia shambulizi lake kwa wana ndoa wasio na watoto,Papa Francis aliongeza kwamba watoto hutajirisha na kusisimua maisha.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani alisikika akisema:''Jamii yenye ulafi ambayo haitaki kuwa na watoto,ambayo inasema kwamba watoto wanachosha,ni mzigo na hatari ni jamii yenye uzuni''.
''Chaguo la kutokuwa na watoto ni la ulafi.maisha husisimuka na kupata nguvu iwapo watu wanazaana.maisha huimarika''.
Source BBC

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni