YESU NI JIBU

Jumamosi, 14 Februari 2015

HALI NI TETE HUKO NCHINI NIGERIA BAADA YA KUNDI LA BOKO HARAMU KUSHAMBULIA JIMBO LA GOMBE:



Kundi la wapiganaji wa Nigeria, Boko Haram, limeshambulia mji mkuu wa jimbo la Gombe, kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Watu walioutoroka mji wa Gombe, walieleza kuwa jeshi linapambana vikali na wapiganaji hao, na kwamba ndege pia zimetumiwa.
Boko Haram waliingia katika vitongoji vya Gombe, baada ya kushambulia mji jirani uitwao Dadin Kowa.
Wapiganaji hao wamewahi kushambulia vitongoji vya mji wa Gombe, lakini hawakupata kujaribu kuuteka mji wenyewe.
Nigeria ilitarajiwa kufanya uchaguzi mkuu, lakini umeahirishwa kwa majuma sita, kwa sababu ya wasiwasi kuhusu usalama.
Chanzo BBC News

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni