YESU NI JIBU

Ijumaa, 10 Mei 2013

UJASIRIAMALI NI NJIA YA KUFUKUZA UMASKINI NA KUKARIBISHA UTAJIRI NYUMBANI KWAKO

 Imeonekana kuwa suala la ujasirimali ni njia peekee inayoweza kumkwamua mwananchi wa kipato cha chini sanjari na wale wanaomaliza shule na kuaanza kusaka ajira bila mafanikiao.
Hili limeonekana kwa vitendo mara baada ya ,wali,i Claudine Simba kuamua kuanzisha training center kituo cha kutolea mafunzo ya mapishi ,maandalizi ya kuanzisha mgahawa,namna ya kuwahudumia wageni wengi na wachache sanjari na uokaji wa mikate na kupamba ikiwepo pia utengenezaji wa vitafunio vya aina nyingi.
Akielezea sababu za kuanzisha kituo hicho bi Claudine amsema lengo ni kuwasaidia wananchi w kipato ncha chini pamoja na wanafunzi ambao walimaliza kidato cha nne na cha sita,wavyuoni na waliop[o manyumbani ambao hawajafanikiwa kuendelea na elimu.
Unaweza kuwasiliana na mwalimu mama Simba kwa ushauri  wa mapishi kupanga meza kuaandaa chakula kwa ajili ya wageni wengi na wachache kwa mawasiliano ya 0754055273 na kwa 0712127419

baadhi ya wanafunzi wakijifunza namna ya kupika vitafunwo ambavyo ni karimati, sambussa na kachori

Huyu ni mrs Celister Shamshely ambaye anaonesha bidhaa ambazo wamekuwa wakitengenezwa wanapofundishwa na mwalimu mama Simba katika kituo ambacho ameanzisha kwa lengo la kuwasaidia watu wa kipato cha chini na wale wanaotamani kuwa wapishi bora  na wataalamu wa vyakula mbalimbali na vitafunwo vya asubuhi.


Hizo ni baadhi ya vitu ambavyo wanafunzi wanatengeneza wakati wa somo la vitendo.

Mwalimu Claudine Simba ambaye amefunga kichwa wakiwaelekeza wanafunzi wake ambaye ni Jesca Mahuta mwenye nguo nyekundu ambaye kwa sasa ni mtaalamu wa kutengeneza karimati na vitafunio mbalimbali na Celista Shamshely ambaye kwa sasa ni mtaalamu wa vitu vingi na kwa sasa anatenda nyingi wakimsikiliza kwa makini
Bestina ambaye amevaa blauzi nyeusi akifurahi mara baada ya kufaulu kutengeneza karimati na skonzi.

mwanafunzi Happy Kimati ambaye pia ni mhitimu wa kidato cha sita aakiwa na mwalimu wake mama Simba akitengeza sambusa na kwa sasa ni mtaalamu wa kutengeneza keki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni