YESU NI JIBU

Alhamisi, 30 Mei 2013

REJOICE AND HOPE MINISTRIES RHM WATOA MATIBABU BURE JIJINI DAR ES SAALAM

Taasisi isiyo ya kiserikali inayoitwa,’Rejoice and Hope Ministries’, -RHM, yenye makao yake makuu nchini       Marekani, kwa kushirikiana na Madaktari nchini, watatoa matibabu ya bure  katika kituo cha Pentekostal Holy Mission maeneo ya Mbezi Jijini Dar es Salaam.
Mwasisi wa Taasisisi hiyo Dk.Rejoice Ndalima amesema kuwa, jopo la madaktari hao kutoka Marekani, watashirikiana na madaktari wa Tanzania na wauguzi kutoa  matibabu ya macho, uvimbe pamoja na magonjwa ya kawaida ambapo watapatiwa dawa bure baada ya kutibiwa.
Sanjari na matibabu hayo, RHM watatoa misaada kwa jamii kama vile wajane, yatima na watoto waishio katika mazingira magumu ambapo misaada hiyo itatolewa Jumamosi hii katika Kanisa la Pentekostal Holliness Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Taasisi hiyo ya RHMI, hutoa misaada mara kwa mara kwa jamii ambapo mwaka jana walikuwa Mkoani Morogoro na walifanikiwa kuwahudumia bure wagonjwa mia tano.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni