Imeelezwa kuwa adui mkubwa wa ukristo si dini nyingine wala mamlaka za kisiasa, bali ni ukristo unaoenea kibaiolojia pasipokuwa na Roho Mtakatifu.
Hayo yameelezwa na Mwangalizi Mkuu wa Wapo Mission International, Askofu Sylivester Gamanywa wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki kumi na saba za Ibada ya ujazo wa Roho Mtakatifu iliyofanyika Jumapili iliyopita katika Ukumbi wa BCIC Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.
Aidha, Askofu Gamaywa amebainisha kuwa, ukristo usioambatana na Roho Mtakatifu ambaye ndiye anayefundisha, si ukristo halisi bali ni imani potofu na kwamba uzao wa kikristo hutokana na Mungu kinyume na uzao wa kibaiolojia.
Huku akishangiliwa na maelfu ya watu waliohudhuria maadhimisho hayo ambayo yameangukia Sikukuu ya Pentekoste, Askofu Gamanywa amesisitiza kwamba kama Mkristo hajaokoka, Mbinguni haingii kamwe hata kama amebatizwa.
Ameeleza kuwa, lengo la maombezi hayo ya ujazo wa Roho Mtakatifu, ni kumtambulisha Mungu katika utendaji wake wa nafsi tatu ambazo ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu na uzao wake wa kiroho.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni