YESU NI JIBU

Alhamisi, 30 Mei 2013

MWANAFUNZI KIDATO CHA PILI KUJINYONGA

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Keko Wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam, Edson John mwenye umri wa miaka kumi na tatu aliyekuwa anasoma kidato cha pili, amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani aliyoitundika kwenye mti.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Mkoani Temeke, Engelbert Kiondo amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo  maeneo ya makaburini Temeke na kijana huyo alikutwa na karatasi yenye ujumbe mfupi  kwamba ameamua kujinyonga kwa kusingiziwa maneno ya uongo.
Hata hivyo, Kamanda Kiondo  alieleza kuwa, sababu  za kujinyonga kwa kijana huyo bado hazijafahamika na mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya Temeke kwa uchunguzi zaidi.
Suala la watu kujinyonga katika jiji la Dar es saalam linaendelea kushika kasi kwani kila kukicha hutolewa taarifa za watu kujinga ama kujaribu kujiua hivyo ni nyema hatua na njia maususi zichukuliwe ili kudhibiti na kuondoa tatizo hilo.

Imeonekana kuwa shetani anasababisha watu kujiua kwa kusingizia vitu mbalimbali kama kuachwa na wapenzi wao wengine magonjwa,shida,kukataliwa jambo ambalo ukichunguza kwa undani sio la kweli ni hila za adui kuwaangamiza wanadamu bila kufikilia toba.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni