YESU NI JIBU

Alhamisi, 30 Mei 2013

VIJANA WATAKIWA KUJIKOMBOA KIUCHUMI KWA KUTUMIA FURSA ZIANAZOJITOKEZA

Wito umetolewa  kwa vijana nchini kutumia fursa  mbalimbali zinazojitokeza katika jamii ili kujikomboa  kiuchumi na kuliinua taifa  kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na  Makamu wa Rais wa Vicoba Bibi  Scholastica  Kevela  alipokuwa akitoa msaada  kwa kikundi cha Jambo Africa Group kwa malengo  ya kuinua  Vijana Jijini Dar es Salaam.
Aidha Bibi Kevela  amesema  vijana ni  muhimu kupewa  kipaumbele  katika Nyanja  mbalimbali ili kumiliki uchumi na  kupunguza utegemezi katika jamii.

Naye Mwalimu wa Ujasiriamali wa Vicoba kitaifa, Bibi  Flora Masalu amesema kuwa, vijana wanapaswa kuachana na dhana ya kuajiriwa na kujiajiri kwa kufanya shughuli  za ujasiriamali.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni