YESU NI JIBU

Alhamisi, 30 Mei 2013

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI TAMASHA LA AMANI NA UPENDO JIJINI DSM


Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la amani na upendo litakalofanyika jijini Dar es salaam, Agosti 28 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habri mwenyekiti wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Hope Family Bw. Omary Kombe amesema lengo la tamasha hilo ni kuenzi amani na upendo hapa nchini.

Aidha Bw. Kombe ameongeza kwamba kutokana nan chi nyingi za kiafrika kukumbwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe wameamua kuratibu tamasha hilo kuihamasisha jamii ya watanzania kutunza amani na upendo sanjari na kuchangisha fedha kwa ajili ya kujengea kituo cha kulelea watoto yatima kiasi cha shilingi milioni 300.

Hata hivyo Bw.kombe amesema jamii inapaswa kuenzi amani hasa ngazi ya familia kwani kukosekana kwa amani katika ndoa ndio chanzo kikubwa cha kuongezeka watoto wa mitaani.
Amani inapotoweka kwenye familia hupelekea watoto na wazazi kuishi katika hali ngumu kiasi kwamba kila kukicha watoto wanaongezeka mitaani na wanaishi kwenye mazingira magumu.
Ni vema kuendelea kuenzi na kusimamia amani na upendo kwa juhudi zote ili kuweza kujenga taifa ambalo linaweza kustawi kiuchumi na kisiasa.  

  

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni