YESU NI JIBU

Alhamisi, 11 Desemba 2014

VITU SABA 7 VINAVYOFURAHISHA AMBAVYO NI VYA MUHIMU KWA MWANAUME:



1.Heshima,

Kitu kikubwa ambacho ni cha muhimu kwa mwanadamu ni heshima,wanadamu wanafanya kila kitu ili waweze kuheshimika na marafiki zao ama watu wa kundi lake.kama ataona kuwa hapewe heshima ya kutosha na wenzake ,anataabika sana.Hata hivyo kukosa kuheshimika inaweza hata kushusha hadhi ya utendaji wa mtu.Hata ukija kwa upande wa kuwa na mahusiano heshima pila mara nyingi hupewa kipaumbele.Pamoja na hayo mara nyingi watu katika mahusiano hawajali sana suala hilo ila kiukweli wale wote ambao huweka heshima mbele mara nyingi wanafanikiwa katika mahusiano yao.
   2.Kukubalika, 
Unaweza kushangaa sana kuona kuwa watu wote hawawezi kuishi bila kukubalika.kwa uhakika kila mtu anahitaji kusifika ama kusifiwa katika yale wanayofanya.Kitu ambacho unaweza kufanya kuwa jasiri kwa mwanaume ama mwanamke na furaha yako itatimilika.Kila mmoja anaweza kuhisi upendo kwa mtu wake,uwe na maneno ya kumsifia mtu wako na utaona tofauti katika maisha yako.
3.Tabasamu lako,

  Je ndugu msomaji unafahamu kuwa tabasamu lako ni la ajabu sana?Linaweza kumfurahisha mtu yeyote hasa mtu wako wa karibu(mpenzi wako).Mpe afurahie joto la tabasamu lako la furaha ,kwa hakika kila mwanaume anahitaji mwanamke jasiri na mwenye matumaini ya mbelenikatika maisha yake ambaye anaweza pia kushirikiana naye mawazo ya furaha pamoja.

Kama msichana anafuraha ina maana kuwa ana mahusiano na mwanaume ambaye anampenda na kumjali,kwa kuonesha furaha kwa mwaume wako itakusaidia kutambua jinsi alivyo mzuri.Kumbuka kuwa kitu kidogo kama hicho ambacho ni tabasamu lako linachangia kwa sehemu kubwa mahusiano yako kwa yule ambaye unampenda.

4.Muda wa kufikiri

 Ukweli ni huu kuwa mwanaume hawezi kufikiria kwa haraka sana,wakati matukio makubwa yanapojitokeza katika maisha,anahitaji muda wa ziada kupfikiria kila kitu.

Wakaiti mwingi inawezekana mume wako anatakiwa kufanya maamuzi magumu na mara nyingi anaahirisha na kufikiria juu aya jambo hilo kwa muda mrefu.Kama sheria ,inamchukua muda kujadili mwanzo na mwisho wa hali halisi ya jambo.Ila kwa wanawake kwa kawaida wanafahamu wanachofikiria juu ya jambo linalojadiliwa.

5.Kuonekana Mrembo,

Hina maana kuwa mwanume wako anaweza kuwaza kile ambacho unafanya wakati akiona kuwa umevaa nguo yako ya kawaida ya nyumbani.

Hata hivyo inawza kumletea furaha ama starehe wakati akikutazama kama unapendeza,lakini sio lazima kutumia vipodozi na kununua vitu vya gharama na nguo pia za gharama.Kwa ukweli kuwa mrembo sio kuonekana kuwa unavaa mitindo ya hali ya juu.Urembo wa asili inakubalika   sanakuliko kingine yeyyote.Mpenzi wake anaweza kuwa na furaha kufamu kuwa unajuhudi ya kuonekana wa kuvutia kwake.

6.Kumpongeza kwa kazi zake.

 

 Kitu kingine ambacho ni ya muhimu kwa mwanaume wako ni kumsifia kwa kazi yake .Jaribu sana kumsifia sana pale anapofanya vizuri.Kama mume wako anafanya kazi kwa bidii kwa lengo la kufikia mafanikio,kumsifia kwako kutamtia moyo kufikia mafanikio makubwa.Haijalishi mume wako ama rafikia yako anafanya nini kumsifia kwako kunamtia sana moyo.Hata hivyo maneno yako yanaweza kumsaidia kuwa na furaha na amani tena haijalishi kama alikwazwa kazinin kwake ama alipokuwepo akifanya kazi ama akisimamia watu,maneno yako ya kusifia yanakuwa ya faraja kwake.

 7.Kicheko chakoUnaweza kuwa na uhakika kuwa kicheko chako kinamfurahisha  mume wako au rafiki yako  na katika njia nyingine tabasamu lako.Bila mashaka ,kicheko chako kinaweza kuleta msisimuko katikakati ya watu wako wa karibu.Inaleta ishara ya furaha na faraja katika maisha yako.kama unatabasamu na  unacheka sana mume wako ama rafiki yako atakuwa anajisikia vizuri kuwa na wewe.

Kiukweli ni vigumu sana kujenga furaha na uhusiano wenye mafanikio na mwanaume kama anakuona kuwa hujaridhika naye na haunafuraha.
Hivyo ndugu msomaji ni lazima ufahamu kile ambacho mume wako ama rafiki yako anapenda na kile ambacho hakipendi na mambo ambayo yanaweza kumfurahuisha.Kwa njia hiyo unaweza kufikia  katika upendo wa kuhitajiana kila mmoja na mwenzake na mtu ambaye ni wa thamani sana katika maisha yako.
Kw hakika katika maisha yako vitu hivi vyote ukivifanyia kazi kwa kuwasiliana na mume wako ama mwenzi wako utafikia katika hatua ya kufanikiwa sana kimaisha na kama umeona unaupungufu wa mojawapo ya njia hizo saba unaweza kumshirikisha ndugu jamaa na rafiki ambaye anaweza kukushauri .
Maoni yako na ushauri unaweza kuweka hapa chini.  

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni