YESU NI JIBU

Jumatano, 3 Desemba 2014

KUNDI LA KIGAIDI LASHAMBULIA MSAFARA WA UMOJA WA MATAIFA MJINI MGADISHU SOMALIA:

Hali tete huko Mogadishu nchini Somalia mara baada mtu anayedaiwa kuwa ni mmoja wa kundi la kigaidi la Al shabaab kujilipua kwa bomu karibu na uwanja wa ndege na kusababisha watu wanne kupoteza maisha .
Hizi ni nyakati za hatari sana hivyo wateule tuwe macho maana ni wakati wa kusimama kila mwamini katika zamu yake na kumlilia Mungu ili aepushe mauaji ya watu ya kila kukicha.

Polisi wanasema kuwa bomu hilo lililipuka wakati msafara
wa magari ya Umoja wa Mataifa mjini Mogadishuhuo ulipokuwa unaelekea karibu na barabara iliyoko karibu na uwanja wa ndege mjin humo.

 Waokoaji katika harakati za kuzima moto.
Mlipuko wa pili iliripotiwa kulenga vikosi vya muungano wa Afrika umbali wa kililomita 25 kutoka mjini humo ingawa taarifa bado ni finyu.
Duru zimearifu kuwa mlipuko huo huenda umesababishwa na mtu aliyejitolea muhanga aliyejilipua ndani ya gari.
Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al- Shaabab mara kwa mara hutumia milipuko ya magari, lakini kufikia sasa halijakiri kuhusika na mlipuko huo.

 Maafisa wa usalama wa kigeni pia walikuwepo katika eneo la shambulizi.
Kundi la Al-Shabab, ambalo limehusishwa na wapiganaji wa al-Qaeda, limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Somalia na katika nchi jirani ya Kenya.
Mnamo siku ya Jumanne liliwaua watu 36 mjini Mandera karibu na mpaka na Somalia.
Hata hivyo bado halijatoa yamko lolote kuhusu shambulizi lililofanywa mjini Mogadishu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni