YESU NI JIBU

Alhamisi, 18 Desemba 2014

SASA BUNGE LA KENYA LAGEUKA KUWA UKUMBI WA MASUMBWI NA KUVUANA MASHATI KWA MUDA MARA BAADA YA WABUNGE KUTOFAUTIANA VIKALI BUNGENI KUHUSU MSWADA TATANISHI WA USALAMA AMBAPO WABUNGE WA UPINZANIWANADAI UNAKIUKA UHURU WA WAKENYA:



Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bungeni  na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.

Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo. 

Seneta Johnston Muthama alijikuta katika sintofahamu mara baada ya suruali yake kuchanika katika mvutano bungeni humo. 
Seneta Muthama alijeruhiwa mguuni

Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyataja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.'

Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.

Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.
Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.
Pia ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.

Mswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia

Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangu mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.
Naibu spika wa bunge Joyce Laboso amwagiwa maji mara baada ya vurugu kuanza.
Kikao cha adhuhuri cha wabunge nchini Kenya, kinaendelea kuzua hisia kali huku wabunge wakiendelea kuvurugana humo. Wabunge hao wanajadili mswada tatanishi wa usalama ambao upande wa upinzani unasema unakwenda kinyume na katiba na kuwanyima wakenya haki yao ya kujieleza.
Mmoja wa wabunge hao wa upinzani amemwagia soda naibu spika Joyce Laboso ambaye alikuwa anasimamia kikao hicho cha kufanyia mswada huo mabadiliko kabla ya kupitishwa.
Spika wa bunge hilo sasa amechukua usukani na kuamuru kutimuliwa kwa wabunge wawili waliokuwa wamezidi vurugu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni