Upendo wa kwanza katika maisha ya kila mtu inaacha nafasi nzuri na kumbukumbu katika maisha ya mtu binafsi.Kama ulishawahi kuachana na rafiki yako wa kwanza ni vigumu ama sio rahisi kuwa naye tena ama kurudisha mahusiano tena naye, ila bado inawezekana kuwa naye katika maisha yako.
Kila mwanadamu kuna kitu anatakiwa kukumbuka na kufuata ni
kutokumbuka kitu ambacho kilishawahi kumuumiza hivyo endelea kuufuatilia kwa
makini mambo sita ambazo unatakiwa kufahamu ili kumrundisha rafiki yako wa
awali ambaye unampenda.
1.Epika
kumtafuta kwenye mtandao wa kijamii (Facebook)
Kama hautaweza kuvumilia
kutomtafuta rafiki yako(mpenzi)wako ambaye mmekosana au mmetofautiana kwenye
mtando wa kijamii Facebook ,basi kuna uwezekano mdogo sana ya kumpata
tena.Kwani Itakuwa vigumu kufahamu kuwa anafanya nini? na anaongea na nani
anawasiliana na nani kwa muda huo.
Hivyo ni vyema kujitahidi kumfungia
katika profile yako maana ataendelea kusababisha maumivu katika maisha yako.
2.Tupilia mbali vitu vyote ambavyo
vinaweza kusababisha ukaanza kumkumbuka.
Njia mojawapo nzuri ya kumpata
rafiki yako wa kwanza ni kutupilia mbali mambo yote ambayo ulikutendea ndivyo
sivyo na hapo unaweza kurudisha upendo wa awali.
Amini usiamini ni lazima utafute
njia ya kufuta kumbukumbu yote ambayo alikutendea ndivyo sivyo.Kama mlitumiana
ujumbe mfupi,barua pepe wakati mmetofautiana ni vyema kufuta hizo jumbe zote
hiyo itakusaidia kumsamehe,ila nji hii inaonekana kuwa ngumu ila ndiyo njia
pekee inayoweza kukusaidia kumsamehe na kutokumbuka.
3. Baadilisha mtazamo wako wa
maisha.
Baadala ya kuendelea kufikiria
yaliyopita ni vyema ukawaza yali yalioko mbele yako.uwe na tumaini jipya,fanya
kazi kwa bidii kuliko kawaida ili kufikia malengo yako.jiweke taratibu ya
kujishughulisha kwa ukichoka kwwa ukweli
ni njia ya kusahau yali uliyokosewa ma yule ambaye umekosana naye.
4. Soma habari ambazo zinasababisha
faraja kwako.
Soma vitabu vya hadithi ambazo
zinaweza kukusaidia kupata furaha ambayo itasaidia kusahau yale yote ambayo
ulitendewa.Unaweza kusoma hadithi kwenye majarida,vitabu na hata kwenye
mtandaona utambue jinsi wengine walivyotatua matatizo na kutambua kuwa kumpoteza
rafiki wako wa kwanza ni jambo la kawaida
5.Fikiria juu mazuri ambayo
ulikuwanayo katika mahusiano yako.
Acha kuwa na kumbukumbu mbaya juu ya mahusiano yako ulikuwa
nayo badala yake fikiria juu ya mazuri ambayo ulikuwa nayo na rafiki yako.Ni
vyema kukumbuka kuwa muda uliyokuwanayo haikuwa bure.
6. Upate muda wa kutosha na marafiki
zako.
Kwa kuhitimisha ni vyema kushikishana uzoefu na marafiki
zako wa karibu na kusikiliza maoni yao na itakusaidia kujisikia vizuri katika
maisha yako.Msaada wao wa kimawazo itakusaidia kujisikia vizuri na kuona kuwa
maamuzi uliyochukua nia sahihi na utaanza kumsahau rafiki yako wa mwanzo.
Kama rafiki yako atakuwa naye amepitia kama hayo ambayo
umepitia unaweza linganisha na kuona kuwa kumrudisha rafiki yako wa mwanzo(mpenzi)
ni jambo ambalo linawezekana.
Nawe
msomaji umempataje rafiki yako wa mwanzo Tafadhali tushirikishe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni