YESU NI JIBU

Jumanne, 2 Desemba 2014

WAKRISTO 36 WAUWAWA HUKO KAUNTI YA MANDERA NCHINI KENYA KARINU NA MPAKA WA KENYE NA SOMALIA:

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa Kenya haitachoka katika vita vyake dhidi ya ugaidi kufuatia
shambulizi lililofanywa dhidi ya wachimba migodi mjini Mandera Kaskazini ya Kenya.
Ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwa taifa baada ya shambulio  lingine lililofanywa na kundi la wanamgambo la Al Shabaab dhidi ya wakenya wasiokuwa na hatia.
 Kundi hilo liliwavamia wachimba migodi 36 waliokuwa katika machimbo ya kokoto mjini Mandera.
Kundi hilo liliwaua wakenya wengine 28 waliokuwa wanasafiri kutoka mjini Mandera siku kumi zilizopita.
Kenyatta amelaani wanamgambo hao wa Al Shabaab kwa kutaka kuigawanya Kenya katika msingi ya kidini na kuwataka wakenya kuungana dhidi ya kile alichokitaja vita dhidi ya ugaidi.
Kenyatta aliwataka magaidi wa Al Shabaab kama wanyama walio na kichaa.
Aliwasihi wakenya kuungana katika vita dhidi ya magaidi.
Siku kumi zilizopita, Al Shabaab waliuwaua abiria 28 waliokuwa wanasafiri kwa basi kutoka mjini Mandera karibu na mpaka na Somalia kuelekea likizoni makwao. Wengi wa waliouawa walikuwa walimu wa shukle za umma. 



 Rais Uhuru Kenyatta amemwachisha kazi waziri wa usalama Joseph Ole Lenku na kumpendekeza waziri mpya wa usalama Joseph Nkaiseri kuchukua nafasi hio.
 Hapa Joseph ole Lenku akisisitiza jambo.
Wakati huohuo mkuu wa polisi nchini Kenya inspekta generali David Kimaiyo amejiuzulu kutokana na shinikizo dhidi yake afanye hivyo kwa kushindwa kukabiliana na utovu wa usalama nchini.

Rais Kenyatta alisema kuwa baada ya mazungumzo na Bwana Kimaiyo alikubali 'kustaafu' mapema kutoka kwa majukumu yake kwa sababu za kibinafsi.
Aliyekuwa mkuu wa polisi Inspekta generali David Kimaiyo.
Rais alitoa tangazo hilo wakati akihutubia taifa kufuatia shambulizi la hapo jana dhidi ya wachimba migodi 36 waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera Kaskazini ya Kenya.

Rais pia alitangaza kuwa amekubali ombi la Generali wa polisi David Kimaiyo kuachia wadhifa wake.

Kimaiyo na Ole Lenku wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo za kuachia ngazi kufuatia kukithiri kwa utovu wa usalama nchini.

Hatua ya kuwatimua kutoka katika nyadhifa zao wawili hao bila shaka litakuwa jambo la kuridhisha kwa wakenya wengi ambao wamekuwa wakilalamikia utovu wa usalama na kuwataka waondoshwe ofisini.

Uteuzi wa Joseph Nkaisery kama waziri mpya wa usalama ni jambo jipya kwani atakuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka kwa upinzani kuwa ndani ya serikali.

Alipokuwa anahutubia nchi,Rais Kenyatta aliwasihi wabunge kuongeza muda wa vikao vyao vya leo ili kumhoji na kumkagua Nkaisery aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya waziri mpya wa usalama na maswala ya ndani ili wamuidhinishe.
Wanajeshi wa Kenya wakiwa wamekusanyika karibu na miili ya baadhi ya waathirika wa mashambulizi ya al-Shabaab kwa wafanyakazi wa machimboni karibu na mji wa Mandera, kaskazini mwa Kenya, siku ya Jumanne (tarehe 2 Disemba). Kiasi cha wapiganaji 20 wa al-Shabaab walivamia machimbo ya mawe, wakawaweka pembeni watu 36 wasiokuwa Waislamu katika kikundi, na kuwapiga risasi za kichwa, ilhali wengine walikatwa vichwa pia, kwa mujibu wa polisi. [PICHA YA AFP / STRINGER]

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni