YESU NI JIBU

Jumatano, 10 Desemba 2014

NI VYEMA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI WALA KUANGALIA DINI,ITIKADI,RANGI WALA KABILA KUSIMAMA NA KUUNGANA KWA PAMOJA NA KUOMBEA TAIFA LA TANZANIA AMANI NA ULINZI WA MUNGU ILI AZIDI KUONEKAKA NA HATA KATIKA MAADHIMISHO MENGI KUWEPO NA UTULIFU KAMA WA SASA PIA KUKUMBUKA UCHAGUZI ILI MUNGU AHUSIKE KIKAMILIFU:

Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara ilifana sana mara baada ya Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwetekuwasili uwanjani na kupigiwa mizinga ishirini na moja na mara baada ya hapo akaanza kukagua gwaride.
Hata hivyo watanzania kwa asilimia kubwa walikuwa
 wakimwaombea mhe.raisi wakati akiwa nje ya nchi 
 kimatibabu na hatimaye amerejea salama na kuhudhuria maadhimisho hayo.



Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum  katika uwanja huo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange.
Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea heshi kwa kikosi cha bendera na kuanza kukagua gwaride.



 Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride lililoandaliwa rasmi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru katika Uwanja wa Uhuru Desemba 09, 2014 Jijini Dar es salaam






 Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa ukakamavu  wakati wa maadhimosho ya miaka 53 ya Uhuru katika Uwanja wa Uhuru Desemba 09, 2014 Jijini Dar es salaam.
 Kutoka kushoto ni Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein  katikati ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwetena kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange.
 kutoka kushoto ni spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe.Anne Makinda wa pili
 Makamo wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd na wa tatu ni  waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda na kulia ni Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na usalama Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Kitaifa wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi katika ni waziri mkuu mhe. mizengo Pinda na kushoto ni spika wa Bunge Anne MAkinda katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.
 Mabalozi wa Nchi mbali mbali wanaoziwakilisha Nchi zao hapa nchini pamoja na Wananchi wakiwa katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

 




 Sehemu  ya viongozi na wananchi waliofika katika Uwanja wa Uhuru Desemba 09, 2014 Jijini Dar es salaam kushuhudia maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania.
Picha na Ikulu blog.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni