Mkurugenzi wa Brothers Academy Ndugu Robart Rwezaura akizungumza jambo na waandishi wa habari.
Na Stelius Sane,
Imebaishwa kuwa elimu ambayo hutolewa
katika mfumo usio rasmi imekuwa msaada mkubwa sana Kwa wale ambao walishindwa
kupata elimu katika mfumo rasmi kutokana Na matatizo mbalimbali ya kifamilia
ama sababu zingine.
Kauli hiyo imetolewa Na mkurugenzi wa
brothers font of academy ndugu Robart Rwezaura wakati akizungumza Na gazeti
hili ambapo alisema kuwa mfumo usio rasmi umekuwa mkombozi wa kielimu Kwa wale
watu walioshindwa kusoma Katika mfumo rasmi.
Aidha aliongeza kuwa kuna baadhi wa
watu hasa watoto wa kike ambao walishindwa kufikia malengo yao kutokana na
ujauzito Kwa kurubuniwa au kubakwa Na kupata ujauzito hali iyoua ndoto yao ya
kielimu.
AlifafAnua kuwa endapo ulishindwa
kupata elimu katika mfumo rasmi usisite kupambana kutafuta elimu maana serikali
imepitisha na kuruhusu elimu kutolewa katika mfumo huo kwa mujibu wa sheria za
nchi.
Akifafanua kwa undani alisema kuwa
Brother academy umejikita kuwasaidia wale ambao hawakupata elimu Kwa mfumo
rasmi,hivyo hutoa elimu ya sekondari Kwa miaka miwili Yaani Qulify test QT na
elimu kidato cha tano Na sita Kwa mwaka mmoja sambamba Na Kwa wale wanaorudia
mtihani wa kidato cha nne Na sita Yaani Resetters.
Pamoja Na hayo wamejikita kutoa elimu
ya computer programu zote,lugha ya kiingereza na kifaransa kutokana na uhitaji
ulipo ndani ya jamii Na wapo mbioni kuanzisha Mafunzo ya kichina.
Ndugu Rwezaura alifafanua kuwa kila
mmoja anaweza kupata elimu pale atakapoamua kusoma hasa pale Brothers maana wao
huwapokea watu waliofanya vibaya katika mitihani Yao ya mwisho na Na pia Kwa
wale ambao hawakufanikiwa kusoma ama kupata elimu kutokana na changamoto
mbalimbali za kimaisha.
Baada ya kuona uhitaji huo Brothers
kama taasisi wamewatafuta walimu wenye taaluma ya ualimu na walifuzu katika
vyuo vikuu wenye mzigo na nia ya kuwasaidia wale walioshindwa kupata elimu
katika mfumo rasmi pamoja Na waliofanya vibaya katika mitihani yao ya mwisho wa
kidato cha nne na sita Na kupelekea kukata tamaa ya kupata elimu na ndoto zao
kielimu kufa.
Aliendelea na kusema Brothers academy
imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya QT na ya kidato cha Sita Kwa mwaka
mmoja katika shule zinazotoa elimu katika mfumo usio rasmi Hali inayosababisha
kuona ndoto ya baadhi ya watu kielimu kuanza kufufuka.
"Mpaka sasatnaendelea kufanya
vizuri hali inayosababisha kuona ndoto za watu kuanza kufufuka maana mpaka Sasa
tuna baadhi ya walimu ambao wameshapata shahada yao ya ualimu kutoka vyuo vikuu
ambao walipitia ama walipata elimu Kwa mfumo usio rasmi hapa Brothers academy
Na Sasa Ni walimu na baadhi wanafundisha hapa"alisema Rwezaura.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni