YESU NI JIBU

Jumapili, 18 Februari 2018

MWIMBAJI WA INJILI ZAKARIA KENYATTA KUZINDUA ALBAMU YA WATAKUHESHIMU KESHO NCHINI CHINA:

Kumtumikia Mungu kwa uaminifu yeye atakuinua kwa wakati wake usipozimia roho maana hutenda zaidi ya akili za wanadamu.

Hii ni baada ya mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania Zakaria Kenyata kutambulisha rasmi albamu yake ya watakuheshimu kesho katika uwanja wa kimataifa nchini China.

Aidha Ndugu Zakaria Kenyatta ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa "Unaweza ukasota zaidi ya miaka 30 kwenye Huduma hakuna hata anae sema hodi hapa lakini Mungu anaweza kukutambulisha dakika moja tu ukasahau kusota kote kwa miaka hiyo usikate tamaa new album ya watakuheshimu kesho ya tambulisha katika uwanja wa kimataifa Leo China.

Mwimbaji Zakaria Kenyatta akitambulisha albamu yake ya watakuheshimu Kesho katika uwanja wa kimataifa wa China.






Watu wa Taifa la China waliofika katika uwanja wa kimataifa kushuhudia utambulisho wa albamu ya mwimbaji wa kitanzania Zakaria Kenyatta.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni