YESU NI JIBU

Alhamisi, 15 Februari 2018

KUWAJALI WANYONGE NA WANAOISHI KATIKA MAISHA NA MAZINGIRA MAGUMU NI KIMUNGU KABISA

Viongozi wa kundi la New vision wakiwa katika picha ya pamoja katika kituo cha watoto yatima ya Bloma.

Mhazini wa kituo cha New Vision Bwana Hamphrey Zebaedaya Isayaakimlisha keki mmoja wa watotot wanaoishi katika kituo cha Bloma.


Mwenyekiti wa kundi la New Vision Bwana Palanjo akiwa na mhazini wa kundi hilo Bwana Hamphrey Zebaedaya Isaya wakimkabidhi mkurugenzi wa kituo cha Bloma foundation zawadi mbalimbali waliopeleka hapo walipowatembelea watoto wa kituo hicho. 


Wanakundi la New Vision pamoja na watoto wao wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha Bloma.
Mwenyekiti wa kundi la New Vision bwana Clement Joseph Palanjo akikata keki na mkurugenzi wa Bloma foundation Anna Fransis Kyando mhazini wa kundi hilo akkipiga makofi na katibu akishuhudia. 

Watoto wa Bloma wakiwa wanasubiri waageni wao.
Mr Mollel wa Betty Funitures akiwa na mwanaye katika kituo cha Bloma walipotembelea na kundi zima la New Vision.
Na Stelius Sane,
Kuwasaidia wengine nia agizo kutoka kwa MUNGU bila kujali dini itikadia wala kabila kutokana na uhitaji wa wengi ndani ya jamii.
Kutokana na hilo kundi la New vision wameamuaa kwenda kinyume na msemo usemao mwenye shibe hamjali mwenye njaa baada ya kuwatembelea watoto wa kituo cha Bloma kilichopo picha ya Ndege Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza na gazeti hili mwenyekiti wa kundi hilo bwana Clement Joseph Palanjo amesema kuwa wameamua kuwatembelea waptoto hao na kuwapa msaada na kula pamoja nao chakula kwa lengo la kujenga upendo na umoja baina ya watoto hao nao wajisikie vizuri na kuona wanajaliwa.
Aidha Bwana Palanjo aliongeza kuwa waliamua kwenda kituo hicho Baada ya kufanya utafiti wa kutosha juu ya vituo mbalimbali vya watoto yatima na walee wanaoishi katika mazingira magumu na ndipo wakaaona kitupo chha bloma ndiyo yenye uhitaji zaidi.
Hata hivyo alisema kuwa wao kama wana New vission walianzisha kundi hilo kwa lengo la kuwasidiana katika kila hali katika shida na raha na pia katika masuala ya maendeleo na kutegemea kuwa baada ya miaka mitano kila mmoja ambaye amejiunga na kundi hilo watakuwa na ushhuhuda mbalimbali ya mafanikio.
Akizungumza na gazeti hili mkurugenzi wa kituo cha Bloma Foundation Anna Fransis Kyando alisema kuwa katika kituo hicho anakutana na changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha maendeleo ya baadi ya watoto wanoishi katika eneo hilo.
Alifafanua kua changamoto kubwa ni mavazi kwa watoto wanaoshi katika kituo hicho pamoja na huduma za Afya maana inagharimu Fedha nyingi pamoja na shule ambazo badhi ya watoto hao wanasoma.
Bi Kyando alisema kuwa katika eneo la kituo anakutana na changamoto ya uzio katika eneo hilo maana kwa sasa yeye ni mstaafu hivyo inamlazimu kufanya shughuli zingine za kumwonezea kipato ili aweze kuwalipa wafanyakazi wanaomsaidia katika kituo hicho.
Aliongeza kuwa ni vyema kwa wasamaria kujitokeza kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na sio kuwa nao nyumbani na kuanza kuwapa tena mateso ambayo ndiyo chanzo cha baadhi ya watoto kukimbia makwao.
Kwa upande wa Mhazini wa kundi hilo la New Vission Bwana Hamphrey Zebaedaya Isaya alisema kuwa kundi lao lina mikakati mikubwa ya kujiletea maendeleo ambapo wao hupata vipato kutokana na kuchangishana wenyewwe katika kundi lao na pia wanamipango ya kusaidiana wenyewe kwa wenye hasa kwa kukopeshana wenyewe kwa wenye kwa riba nafuu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni