Na Stelius Sane,
Imebainika kuwa kila mmoja akikomboa wakati badala ya kwenda
na wakati atafanikiwa katika maisha yake kiuchumi,kiafya,kisiasa na hata kiroho
kutokana na kuwa katika wakati sahihi wa kile anachokifanya.
Hayo yalisemwa na mchungaji Bernard Jomalema wa huduma ya
wapo mission International wakati akizungumza na gazeti hili jijini Dar es
salaam ambapo alisema kuwa kuna tofauti ya kukomboa wakati na kwenda na wakati
ila asilimia kubwa ya watanzania hawajatofautisha na ndiyo maana kuna malalamiko
na manung'uniko ndani ya jamii.
Mchungaji Jomalema alisema kuwa kila mmoja akikomnboa wakati
malalamiko katika sehemu za ibada,sehemu za kazi na hata katika familia
itapungua kama sio kwisha kabisa maana kila mmoja atafahamu anatakiwa kufanya
nini na kwa wakati gani.
Aidha aliongeza kuwa ili Mungu amwinue mwanadamu katika
maisha yake ni pale tu atakapokomboa wakati maana kuna baadhi ya watu ama
waumini pamoja na wananchi wanalalamika ila bado wao wenyewe wanasababisha
maisha kuwa magumu.
kukomboa wakati ni pale ambapo unafanya kinachotakiwa kwa
wakati sashihi na kwa muda muafaka na sio kuwa unawasili sehemu ya majukumu na
kuanza kufanya majukumu mengine kinyume na yale yanayohitajika kufanya kwa muda
ule ulipo.
Ni kweli kuna mambo hayaendi ila sio kwamba sababu ni Mungu
ama shetani ila ni wewe mwenyewe umekuwa kikwazo cha mafanikio ya maisha yako
sasa ni wakati wa kufunguliwa ili utambue yale ambayo Mungu anataka ufanye
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni