Askofu mkuu wa kanisa la Faith Community Pentecoste Church
(FCPC) lililopo Mbezi Maramba mawili jijini Dar es salaam,Barthelomeo Sheggah
amewataka wakristo kuhibiri juu ya ufalme wa mbinguni ikiwa ni njia pekee ya
kulijenga kanisa la Mungu kulingana na misingi ambayo Yesu alituwekea tangu
mwanzo
Akizungumza katika Ibada wiki iliyopita Askofu Sheggah
ameuelezea kuwa ufalme huo ni katika ulimwengu ambao hauonekani kwa macho ya
kawaida bali kanuni zake zipo na zinafundishika
Askofu Sheggah alisema watu wanapaswa sana kufahamu kanuni za
ufalme huo ambapo ili kila mmoja aweze kuzitenda kanuni hizo anahitaji hekima
kutoka kwa Mungu.
Alisema kanisa limepoteza ufalme na inatupasa kuurudisha ambapo
aliitaja njia moja wapo ni kutubu
"Yesu alianza kuhubiri juu ya ufalme wa mbinguni umekaribia
lakini pia Yohana nae alihubiri vivyo hivyo tangu mwanzo ambapo aliwataka watu
kutubu" alisema Askofu Sheggah.
Aidha alithibitisha maneno hayo katika vitabu mbalimbali kwenye
Biblia na kutolea ufafanuzi juu ya neno 'Umekaribia' kuwa lilimaanisha wakati
umefika au upo sasa ambapo akautambua uelewa huo kuwa ni wa kimapinduzi.
Askofu Shaggah aliongeza kuwa sasa imefika wakati hata serikali
haiwezi kuomba msaada kwa viongozi wa dini kutatua baadhi ya mambo
kutokana na kanisa kupoteza ufalme.
"inatupasa na ni muhimu kuwa na ufalme kwani hata zamani
viongozi wa nchi walipofika wakati wanashindwa kutatua mambo waliwatafuta
viongozi wa dini lakini kwetu hakuna na hilo linachagizwa na kuupoteza
ufalme"alisema
''Ipo haja ya kubadilika katika mwaka huo na kuanza kutafuta
namna ya kuurudisha ufalme kwa kuhubiri sana ingawa mengine ni muhimu lakini
hili la ufalme litarahisisha mengine yote"aliongeza Askofu Sheggah.
Alitolea mfano Yesu alikemea pepo kwa kuwawekea mikono wenye pepo
nao pepo wakatii na kutoka lakini sasa Wachungaji, Manabii na hata Mitume
wanakemea hata saa matatu pepo bado hatoki, hii ni kwa sababu tumekosa ile
nguvu ya kifalme.
"Tukiwa na ufalme kila kitu kitakuwa rahisi maana nguvu ya
ufalme huo hakuna wa kuufananisha nao kwani tunakuwa tumebeba mamlaka ya
kimungu" Alimalizia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni