Askofu na mchungaji Kiongozi Selestine Kato akifundisha watumishi wa Blessing Community kwenye Kongamano liloandaliwa na kanisa hilo kwa lengo la kuwanoa watumishi wake
Mtangazaji wa Wapo Radio na mwandishi wa gazeti Msemakweli pia mmiliki wa Blog hii akifundisha umuhimu wa watumishi wa Mungu kutumia vyombo vya habari na mawasiliano kwa ujumla.
Merrystela Kato katikati akiwa na baadhi ya watumishi katika kongamano la watchungaji na watendakazi wa kanisa la Blessing Community wakiwa katika ibada ya kusifu na kuabudu.
Mwalimu Menrald Mtitu Kutoka ICM akiwafundisha wachungaji na watumishi waliohudhuria kwenye Kongamano huko Mpera Kisemvule.
Ni wakati wa kumwabudu Mungu katika Roho na kweli ndiyo alivyonekana askofu Kato akifanya kwenye kongamano la wachungaji na watumishi wa kanisa la Blessing Community
Na Stelius Sane,
Imebainishwa kuwa mwamini yeyote
anapokomboa wakati anafanikiwa kufikia viwango vya juu kiroho na kimwili hali
ambayo itasaidia hata wanaomzunguka kuwa na furaha ya kumtafuta na kumtumikia
Mungu.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na mchungaji
Bernad Jomalema wakati akiwafundisha baadhi ya wachungaji na watendakazi wa
kanisa la Blessing Community iliyopo
chini ya askofu Selestine Kato waliokuwa kwenye kongamano la kujifunza masuala
mbalimbali ya kihuduma na kijamii pia.
Aidha Askofu na mchungaji Jomalema
alisema kuwa kumtumikia Mungu si mateso na sio mzigo mzito kama wengine
wanavyowaza ila ni kazi nyepesi sana kama umeitwa kweli na MUNGU Kumtumikia na
sio hisia zako zinakusukuma,kama ni hivyo utaona kumtumikia Mungu ni mzigo tena
mzito sana.
“Leo ninyi watumishi na viongozi
mmekusanyika hapa lengo sio kwamba hamfahamu kutumika hapana ni kuinuana na
kutiana moyo katika utumishi wenu mlioitiwa na Mungu katika maeeneo yenu ya
huduma,hivyo ni vyema kila mmoja kusimama katika nafasi yake kama yeye
kumtumikia MUNGU wake kwa bidii,”alisema mchungaji Jomalema.
Kwa upande wa askofu kiongozi wa
kanisa hilo la Blessing Commuty askofu Kato alisema kuwa yeye anafurahishwa
sana opaleanapoona watu wakimtumikia Mungu kwa bidii katika maisha yao na kumzalia
matunda yatakayodumu.
Askofu Kato alisema kuwa kwa sasa
wanampango wa kuwafikikia wale ambao hawajafikiwa na injili ya Yesu Kristo
katika maisha yao nao watafunguliwa na kuwa salama maana kuna watu wengi
wamefungwa katika maisha yao na vifungo mbalimbali vya magonjwa,mapepo na hata
rohonza umaskini imewaklia kiasi kwamba kila wanalolifanya hawafanikiwi sasa
inabidi kuwafikia ili Bwana Yesu awafungue na kuwaweka huru mbali na mateso na
dhambi.
“Kwa sasa tunamshukuru Mungu maana
tunawafikia baadhi ya watu hasa katika maeneo ya Malela tunamuona Mungu
akiwahudumia na kuwainua waliofungwa kwa viwango vya juu sana,”alisema Askofu
Kato.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni