Imebainishwa kuwa kulinda moyo ni ia mojawapo ya
kuepukana na magonjwa yanayoweza kushambulia mwili sanjari ya kuepukana na vifo
vinavyotokana na magonjwa ya moyo.
akifundisha somo la namna ya kulinda moyo na Bi Monica
lawrent ambaye yupo chini ya huduma ya mwana
wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kilichopetea inayongozwa na mtumishi Saimon Jonath iliyopo mkoani Morogoro ambapo
amesema kuwa ili kuepukana na magonywa yanayoshambulia moyo na kuonekana katika
mwili na roho ni kulinda moyo kama biblia inavyosema.
Akinukuu kitabu cha Mithali 4:23 amcha kimeandikwa
kuwa linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;maana ndiko zitokako chemchemi za
uzima,
Aidha Bi Monica alielezea maana ya Moyo na kazi yake na unahusikaje? na uzima wako wa roho na mwili? ambapo alianza
kwa kusema Moyo ni kiunganishi cha roho na mwili.
"Haujui kuwa moyo unaposhindwa kufanya kazi roho
haiwezi kuishi ndani ya mwili tena? Yaani mauti humkuta mtu huyo na matokeo ya
moyo yanaweza kuleta madhara ktk roho yako, kama mithali15:13b inavyoelezea
kuwa bali kwa huzuni ya moyo roho upondeke."Alisema Bi Monica.
Aliongeza kuwa mtu mwenye moyo wa namna hii roho
yake haiwezi kuwa na nguvu hata ya kuomba, pia matokeo yake huleta madhala ktk
mwili,sawa na kitabu cha mithali 14:30 ilivyoandikwa kuwa moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; bali husuda ni ubovu wa
mifupa.
Mtu anapokuwa na matatizo ya moyo humpelekea kuwa
mgonjwa wa mwili hata kulazwa, na hii huonekana dhahiri kwa mtu mwenye presha.
Hata hivyo aliongeza kuwa jambo ambalo unaliwaza
ktk moyo ndiyo linaloleta matokeo ktk mwili au ktk roho yako,kama mithali 6:18 inavyoelezea
moyo uwazao mawazo mabaya;miguu iliyo myepesi
kukimbilia maovu;
"Sasa tunapata kuona kuwa nikwanini
tuliambiwa tulinde sana moyo kuliko hata mwili,ni kuhakikisha moyo wako uko
salama wakati wote,kutengeneza moyo si kazi ya MUNGU wala sio ya jirani yako
bali inakuhusu wewe",alisema Bi Monica.
Hivyo aliendelea kuwa kusema kuwa mwenyewe,ukiuandaa moyo ktk kusamehe ni wewe
mwenyewe hata kama utakuwa umekosewa
kosa kubwa kiasi gani,hautàlibeba moyoni bali utaliachilia.
Akinukuu kitabu cha mithali 16:1a alisema kuwa maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; jitahidi kuuandaa vyema
moyo wako ili kupata majibu bora ktk mwili na ktk roho.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni