YESU NI JIBU

Jumamosi, 2 Aprili 2016

MCHUNGAJI ASALIMIKA NA MKE WAKE KATIKA AJALI MBAYA NA KUPOTEZA WATOTO WANNE:

Katika maisha ya mwanadamu kifo imeonekana kama fumbo ambalo limejificha ila kiukweli wateule hupata tarifa maana MUNGU anasema hatafanya jambo bila kuwajulisha watu wake.
Kwa sababu hiyo ni vyema wanadamu tuishi maisha ya kumpendeza Mungu ili tuweze kuishi maisha ya amani na furaha maana wanadamu watafahamu wanayemtumikia.
Maana kwa akili ya kawaida ya kibinadamu wanadamu wangefahamu siki ya kufa wangeishi maisha  ya namna gani.

Labda inawezekana wasingesoma,labda wasingejenga nyumba,labda wasingeoa na kuolewa,labda wasingezaa watoto na yamkini wasingenunua magari wala kusafiri kwa kutumia vyombo vyao vya usafiri ila kwa asilimia kubwa inabaki kuwa fumbo!
Pamoka na hayo siku ya jumanne ya tarehe 26 march 2016  ilikuwa siku ngumu na mbaya ambayo itabaki kuwa kovu kwa maisha ya mchungaji Pastory Michael Kajembe mwenye umri wa miaka 51 ambaye ni mchungaji wa TAG-Ebenezer (Dodoma)Mwanataaluma mahiri wa Theolojia,na Mwalimu wa Chuo cha Biblia Dodoma (Central Bible College, zamani AGBC) na familia yake,Kanisa la TAG kwa ujumla,ndugu jamaa na marafiki...baada ya kupata Ajali ya Gari akiwa na familia yake, asubuhi ya saa moja na robo katikati ya Mtera na Mpunguzi,Mkoani Dodoma na Kupoteza Watoto wake Wanne kwa pamoja Junior, Isaac, Gabriel na Glady katika ajali hiyo.
Mchungaji Pastory Kajembe na Mama, Bwana amewaponya,bado wanahitaji maombi maana nao wamepatwa na Majeraha na wanaendelea na matibabu...
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoani Dodoma David Mnyembuga alisema ajali hiyo ilitokea baada ya gari alilokuwa akiendesha mchungaji huyo kuacha njia na kupinduka.
Aliongeza kuwa baada ya ajali hiyo watoto wanne wa mchungaji huyo walipoteza maisha ambapo alifafanua kuwa watoto wawili walifia eneo la tukio na wengine wawili walifia hospitalini wakipatiwa huduma katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.
 mchungaji Pastory Michael Kajembe na mke wake na watoto wao enzi za uhai wao.
 Gari waliyokuwemo watumishi wa Mungu na watoto wao. Picha na habari Matthew Sasali

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni