YESU NI JIBU

Ijumaa, 8 Aprili 2016

IBADA YA MAOMBI NA MAOMBEZI YA KUFUNGULIWA NA KUWEKWA HURU NDANI YA KANISA LA EAGT CITY CENTER ILIYOPO MTONI MTONGAJI TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM:

 Askofu Josephat Katunzi akifundisha neno la Mungu katika kanisa la EAGT City Center iliyopo Mtoni Mtongani.
 akifafanua neno ndani ya kanisa la EAGT.

 Pokea kwa jina la Yesu mtenda miujiza.
 Maombi na maombezi yakiendelea ndani ya kanisa hilo la EAGT City Center.


 Waliovamiwa na mapepo wakifunguliwa kwa jina la Yesu.
 pokea uponyaji kwa jina la Yesu.
 Zoezi la maombi na maombezi limeanza kwa jina la Yesu.

 Inua mikono juu kwa ajili ya kufunguliwa katika matatizo yako unayopitia .
Mtu mmoja mabye aliletwa akiwa hajiwezi na kuombewa na mtumishi wa Mungu askofu Katunzi.

Imeelezwa kuwa katika maisha ya waumini kuna vizuizi mbalimbali ambavyo vinasababisha muumini asifikie malengo yake  hasa kiroho na kimwili.

Kauli hiyo imetolewa na askofu wa jimbo la temeke na pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT City Center  iliyopo  mtoni mtongani jijini dar es salaam.
Akifundisha somo la MAOMBI YA UKOMBOZI UFUNGUO WA sehemu ya 16 (PASAKA) ambayo ni KUFUFUKA NA KUHUISHWA,alisema kuwa kuna vizuizi ambavyo vinawakwamishwa watu katika maisha yao ya kila siku na vinaondolewa na nguvu za ufufuo ambayo Bwana Yesu ndiye anaweza tu kuwafungua.
Akinukuu kitabu cha  hosea 13:14 kunawatu wamefungwa katika maisha yao katika kazi nyumbani na hata katiika familia zao
Yohana 11:1-44
Yesu ndiyo ufufuo na uzima akiingia ndani ya maisha yako unawekwa huru katika maisha yako kazini kwako na hata katika chochote unayofanya.
inawezaka ulikuwa unaumwa umeteseka umepitia katika maisha magumu lakini mpaka sasa yesu anafufua kila kitu katika maisha yako maana yeyey ndiye ufufuo n uzima.
kuna mambo ambyo yameshindikana katika maisha ya mwanandamu ila kwa mungu yanawexzdekana maana muujiza hauwezi kuwa muujiza kama mwanadamu anaweza kuufanya katika maisha yake.
Hata hivyo alisema kuwa kuna watu wamefungwa na udini na udhehebu wake na bado Mungu anawahitaji kuwafungua katika maisha yao na ndiyo maana nimeamua kuanzisha ibada ya jumamosi.
ili kufanikiwa kuwa vuta wateja na kuwaweka katika maisha yao inatakiwa uweke mikakati na mbinu ya kuwavuuta ili waweza kuwepo katika kundi la kufunguliwa na kuwekwa huru katika maisha yao.
Kuna waumini wangi wanamalka ya kutumia ila hawajui jinsi ya kutumia mamlaka hiyo maana katika maisha ayako unaweza ukawa na elimu kumbe imekufa biashara kazi na hata ndoa imekufa sasa unamamlaka ya kuita katika maisha yako na kuitika na kufunguka katika maisha yako.
Bwana Yesu alipoenda kwa akina matha na Mariamu ambayo ndugu yao lazaro alikuwa yesu aliwaambia tu kuwa toeni jiwe na kuita lazaro toka nje naye akatoka sasa anawe unaweeza kuita  mambo yako na itaoka katika kundi ambalo uliwekwa.
kunawatu ambao walilaaniwa na shangazi na watu wao lakini kwa Mungu hayo yote yanawezekana nawewwe unatakiwa useme wakati ukishika sadaka yako ,maana Mungu amekupa neno la kusema ili kufufua mambo yako yaliyokufa NA kuwa huru.

Yesu alisema nitaweka roho yangu juu yao nayo inatwaweka watu wangu juu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni