YESU NI JIBU

Jumanne, 26 Januari 2016

MTUME NA NABII BETHANIA SIMON MWASISI NA MBEBA MAONO YA OPERATION NIBEBE NAMI NIKUBEBE UPOKEE YOTE.









Mtumishi wakweli wa Mungu hapaswi kuficha mafunuo yake,anapaswa kuyatangaza maana sio bangi bali ni habari njema kwa watu wote,labda wanao ficha hawayaamini mafunuo yao kuwa ni ya Mungu Yehova Bwana wangu,waweke wazi kama mimi hapa.
Ufunuo huu ni kama unaleta kichekesho,na kwa wale walio mwilini huenda wasinielewe kabisa,lakini ni ufunuo wenye maana kubwa sana kibibilia.
Nime anza operation nibebe na mimi nikubebe,au tubebane ili tufike,kama watu hawawezi kubebana basi maana yake ni kwamba mtasimama milele na hamtakuja kutembea ili mfike kule mtakako kwenda.
Tokea huu ufunuo uje kupitia mimi hapa,watu hufunguliwa pindi ninapo kuwa nahubiri huku nimebebwa dede juu kwa juu,kanisa limeanza kuongezeka kwa kasi kubwa,watu wanatoa shuhuda za ajabu sana.
Nashauri watumishi waumini na wa Tanzania wote muanze kubebana juu kwa juu,na tuweke wazi mafunuo yetu maana sio bangi wala meno ya tembo.
 Karibuni mezani Maana wa Tanzania wengi huongozwa na hofu badala ya kweli iliyo mioyoni mwao.





Waumini  wakiwa katika ibada

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni