Watanzania wametakiwa kuliombea taifa amani ili liendelee kudumu
katika hali ya utulivu upendo na mshikamano na kuepukana na machafuko
yanayoweza kutokana na viongozi kushindwa kuongoza kwa haki na hivyo kujenga
chuki miongoni mwa wananchi wake.
Akitoa salamu za mwaka mpya kwa waumini wa kanisa katoliki katika
ibada ya uzinduzi wa parokia mpya ya mbarali askofu wa jimbo katoliki la Iringa
ambaye pia ni rais wa baraza la maaskofu katoliki nchini TEC,Mhashamu askofu
Tarcisius Ngalalekumtwa amesema watanzania wana kila sababu ya kumshukuru
mungu na kuendelea kuombea viongozi wa nchi kutenda haki kwa watu wote
ili amani iendelee kuwepo nchini.
Awali akisoma risala ya waumini wa parokia ya mbarali katibu wa
Parokia hiyo Bwana Francis Katuli amemshukuru askofu huyo wa jimbo la Iringa
kukubali kuigawa Parokia ya Rujewa na kuzaa parokia ya pili ya mbarali kwa
lengo la kurahisisha huduma za kiroho kwa waumini wake na kufanya jimbo la
iringa kufikisha idadi ya Parokia 38.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni