Mwenyekiti wa nyumba ya wahudumu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza ,mchungaji Andrew Kashilimu akisoma tamko la wachungaji.
Askofu huyo ni wa pili kutimuliwa na
uongozi wa kanisa hilo baada ya mwaka 2007 aliyekuwa Askofu wa dayosisi hiyo,
John Changae na yeye kufukuzwa kutokana na matumizi mabaya ya madaraka kitendo
ambacho kinaonesha taswira mbaya kwenye kanisa hilo.
Pia Askofu Kwangu
aliyedumu kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minane, katika uongozi wake
alishawahi kutuhumiwa na waumini wake kuwa anajihusisha na dini ya Freemasons
huku wengine walikuwa wakimtuhumu kwamba anatumia nguvu za giza.
Askofu Kwangu na wenzake
wanne wanatuhumiwa na kanisa hilo kwa ubadhilifu wa zaidi ya Sh. 600 milioni
pamoja na kuendesha kanisa hilo bila kufuata kanuni na taratibu za kanisa hilo
kitendo ambacho kimesababisha kutimuliwa kwake.
Askofu Kwangu,
anatuhumiwa na upotevu wa Sh. 500 milioni ya shule ya kimataifa ya Isamilo,
kuuza gari la dayosisi hiyo, kufukuza wafanyakazi wa kanisa hilo na kusababisha
wadaiwe Sh. 60 milioni, kujipatia kiasi cha zaidi ya Sh. 15 milioni kutoka kwa
Mhasibu wa kanisa, Sam Wisa, bila kibali.
Akisoma tamko la
kumfukuza kazi, Mwenyekiti wa Nyumba ya Wadumu kutoka DVN, Andrew Kashilimu,
amesema askofu huyo ameisababishia hasara kanisa hilo zaidi ya Sh. 600 milioni,
kutokana na kufanya kazi bila kufuata kanuni na taratibu.
Amesema kuwa askofu
Kwangu amekiuka viapo vya uaskofu, katiba ya jimbo, katiba ya DVN na amekiuka
maadili na kanuni, kuendekeza matabaka ndani ya wahudumu na waumini, kutoa
ajira ndani ya DVN kinyume na taratibu za kanisa.
Amesema katika kikao
kilichoketi Septemba 1 mwaka jana, kilithibitisha mambo hayo na kukubaliana
kwamba Askofu huyo ajiuzulu kwa afya ya kanisa la Mungu lakini alikaidi maagizo
hayo mpaka kutoka kwa tamko hilo.
“Askofu (Boniphace
Kwangu) ametumia vibaya madaraka yake na alikuwa anatumia vibaya mali na fedha
za kanisa, kwa hali hiyo tusingeweza kuwa na kiongozi wa namna hiyo,” amesema
Kashilimu.
Mmoja wa waumini ambaye
alikubwa na fagio la Askofu, Kwangu, Edwar Kibiti, amesema kwamba kutimuliwa
kwa kiongozi huyo wa kiroho katika kanisa hilo kutasaidia kurudisha matumaini
kwa waumini walio wengi.
Kibiti ambaye pia ni
Mchungaji amesema kuwa walipokuwa wakijaribu kuhoji sababu za Askofu Kwangu
kuuza mali za kanisa ikiwamo gari alilochangiwa na waumini alikuwa akiwafukuza
watu waliotaka kufahamu suala hilo.
“Tulipokuwa tunahoji
matumizi ya mali za kanisa tulichokuwa tukiambulia ni kwenda polisi na wengine
wafukuzwa, huyu (Askofu Boniphace Kwangu) alikuwa anafanya kazi kwa majungu na
mpaka anaondoka alishafukuzwa wachungaji 19,” amesema Kibiti.
Amesema kuwa baada ya
askofu huyo kuona wachungaji wazawa wanaanza kumfuatilia alianza kutafuta
wachungaji wengine kutoka nchini mbalimbali hususani ni kutoka Rwanda, ili
kuficha maovu yake anayoyafanya.
Mmoja wa Waumini,
Joycelyn Juma, amesema kilichomghalimu askofu huyo ni upungufu wa mambo ya kiuongozi
ambayo yamechangia kusababisha kuwepo kwa mwanya wa wizi wa mali na fedha za
kanisa hilo.
“Kiufupi nimefurahi sana
kwa sababu mambo ya ufisadi ama wizi wa fedha haviendani na mambo ya Mungu na
nimefurahi kuona suala hili limefikia mwisho na sasa tutakuwa na amani,”
amesema Juma.
Sanjali na kufukuzwa
kazi ya Uaskofu DVN, pia uongozi wa kanisa hilo limemfungulia kesi Askofu
Kwangu na wenzake wanne, Katibu wa Bodi, James Mtaritinya, Mhasibu wa Shule ya
Isamilo, Sam Wisa, Samson Maganga na John Magawa.
Kesi iliyofunguli ni
Januari 10 mwaka huu, Mw/Rb/265/2016 ambalo ni jalada la uchunguzi kwa
watuhumiwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni