Wito
umetolewa kwa wanawake wajane nchini, kufunguka kiroho, kujiamini na
kutojidharau ili waweze kujijengea uwezo wa kiuchumi kupitia ujasiriamali na
kulea vyema watoto wao.
Hayo
yameelezwa na Mwenyekiti wa Huduma ya Elishadai inayosimamia wanawake wajane,
Mwinjilisti Agusta Ernest Kitea kutoka Kanisa la Gosheni lililopo maeneo ya
Ilala Mchikichini wakati akizungumza kwenye Kongamano la siku moja la wanawake
wajane lililofanyika katika Ukumbi wa Parokia ya Msimbazi Jijini Dar es Salaam.
Mwinjilisti
Agusta ambaye alifiwa na mumewe miaka saba iliyopita huku akimwachia mtoto
mchanga amebainisha kuwa, huduma yake inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo
ukosefu wa fedha.
Kongamano hilo la pili kufanyika
nchini, limehudhuriwa na takribani wanawake 180 ambapo kongamano la kwanza lilifanyika Julai
16 mwaka jana katika Ukumbi huo na kongamano lingine linatarajiwa kufanyika
Desemba 18 mwaka huu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni