YESU NI JIBU

Jumamosi, 28 Julai 2012


Imeelezwa kuwa ni vyema wanadamu kumnyenyekea Mungu katika maisha yao ya kila siku ili waweze kuishi maisha ya amani na usalama katika maisha yao sambamba na kuifuata njia za kweli.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya kanisa la EAGT Saranga jijini Dar es salaamu mchungaji Florian Katunzi amesema kuwa imetosha kwa mwanadamu kutenda dhambi katika maisha yake kwani tangu mwanadamu kuanza kutenda dhambi hajawahi kutosheka katika maisha ya dhambi
Aidha mchungaji katunzi amesema kuwa haijalishi kuwa unafanya kazi ya namna gani kama hujaokoka ni kazi bure maana wapo wengine wanaitwa wafia dini kwani wanakuwa walevi na bado wanakwenda makanisani na wakati mwingine anakwenda kwa waganga na wachawi huku akisema wanamwabudu Mungu huku maisha yake hayampendezi Mungu.
Pamoja na hayo aliongeza kusema kuwa ni vyema kumtafuta yesu katika maisha yako na katika makusanyiko mbalimbali kumekuwepo watu ambao  wanakuwa kama ni wasindikizaji katika maisha ya dini na kuendelea kujificha kwa kivuli ya dini na kuendelea kutenda makosa na dhambi.
Hata hivyo mch.Katunzi amesema kuwa wapo wengine wamekuwa wakifuga majini katika nyumba zao badala ya kufuga mifugo na wanyama wengine wa kufugwa badala yake wanafuga majini kwa lengo la kuwatesa wanadamu wengine .
“Bila Yesu mwanadamu huwezi ukakwepa majini na wachawi sambamba na wachawi  bila kumpokea bwana Yesu kama bwana na mwokozi wa maisha yako bila hivyo utaendelea kuteseka katika maisha yako ya kawaida kama wanadamu wengine hivyo ni vyema umkubali Yesu katika maisha yako” alisema mchungaji Katunzi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni