YESU NI JIBU

Jumapili, 29 Julai 2012

WAISLAMU WA RUFIJI WAKWAMISHA UJENZI WA KANISA NA KUTISHIA KUCHOMA


 
Katika hali isiyo ya kawaida waislamu katika eneo la utete Wilayani Rufiji Mkoani Pwani wamezuia ujenzi wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania licha ya kuwepo kwa vibali vya ujenzi wa kanisa hilo vilivyotolewa na serikali ambapo wametishia kuwa litaendelea kujengwa watalilipua kama likiendelea kujengwa kinyume na matakwa yao.
Kutokana na hali hiyo uongozi wa kanisa hilo chini ya mchungaji Agnes Maliwanga umeiomba serikali ya jamhuri ya muungano waTanzaniakuingilia kati unyanyasaji unaofanywa na waislamu dhidi ya kanisa hilo mbele ya macho ya watendaji wa wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa Mch. Maliwanga kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo kinamilikiwa kihalali kwa miaka kumi hivi sasana kwamba ni eneo halali kwa ajili ya ujenzi wa kanisa ,likiwa tayari limepimwa na kuidhinishwa na idara ya ardhi ya wilaya ya Rufiji.
Mchungaji Maliwanga alisema kuwa ujenzi wa kanisa hilolilianza toka mwaka 2008lakini ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Rufiji kupita barua yenye kumbukumbu nambari BA73/165/01/23 ya februari 2/11/2011 iliyosainiwa na kaimu katibu tawala wa Wilaya hiyo bwana Milongo Sanga iliwasilishwa kwake akitoa amri ya ujenzi wa kanisa hilo kusitishwa.
“Baada ya kuzuiwa ujenzi tulifuatwa na waumini tunaowafahamu kuwa ni waumini wa dini ya kislamu  wakitamba kuwa wao ndio wameshinikiza kanisa bhilo lisijengwe kwenye eneo hilona badala yake wanata eneo hilo liongezwe kwenye eneo la shule ya mapinduzi ” alisema mch. Maliwanga.
Aliongea kuwa uongozi wa kanisa hilo lilishangazwa na jambo  hilo kwa vile shule hiyo ya msingi imetengewa eneo kubwa la kutosha ambapo alisema waumini hao walifikia hatua ya kutamba hadharani kuwa ikiwa ujenzi wa kanisa hilo utaendelea watahakikisha kuwa linalipuliwa na kuchomwa moto.
Kwa uchungu mchungaji alisema kuwa hali hiyo inapelekea waumini wa kanisa hilo kuwa na hofu wakati wa kuabudu kwani pamoja na kutoa taarifa katika kituo cha polisi cha Utete lakini majibu waliopewa yaliwasikitisha.
Wakati waumini hao wa dini ya kiislamu wakitishia kuchoma moto kanisa la EAGT Utete matukio ya uchomaji wa makanisa nchini yamekuwa yakiripotiwa kutokea mara kwa mara ambapo tangu mwaka 1984 tayari makanisa 46 yamechomwa moto na waumini wa dini ya kiislamu.
Takwimu zinaonesha kuwa makanisa 26 yamechomwa visiwani Zanzibar wakati 20 yameteketezwa kwa moto katika mikoa kadhaa upande wa Tanzania bara,wakati hiyo ikiendelea hakuna taarifaza misikiti kuchomwa moto.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni