YESU NI JIBU

Jumapili, 14 Februari 2016

SHIMO LISIFUTE NDOTO YAKO


Siku zote mwenye ndoto hakosi vikwazo, vikwazo vitainuka vingi sana ili kufuta ndoto ya mwenye ndoto maana shetani anajua kuwa ndoto ikifutika tu basi haitoweza kutimia maana nguvu za kutimia kwa ndoto zipo ndani ya mtazamo wa mwenye ndoto kupitia uwezo wa mungu juu ya wakati sahihi uliyoamriwa.

Yusufu alipoota ndoto ndugu zake wakatafuta jinsi ya kuifuta ndoto yake kwa kumtupa kwenye shimo yawezakana kabisa na wewe ukatupwa kwenye shimo na shetani ili ufute ndoto yako najua ndani ya shimo kuna giza huoni njia lakini pia kuna kuto kuwa na uhuru maana ukigeuka kulia kuna ukuta kushoto kuna ukuta mbele kuna ukuta na nyuma kuna ukuta hakuna njia ya kutokea. Ni kama yusufu hakuona njia lakini kuna kitu kimoja kilimsaidia yusufu nacho ni hiki kuto kufuta ndoto yake oooh hii ni siri kubwa yusufu aliijua ndiyo maana aliopotupwa kwenye shimo alitumbukia mule shimoni na ndoto yake maana alijua kuwa kusudi la shimo ni kufuta ndoto sasa na ndoto inanguvu kuzidi shimo hivyo shimo haliwezi kuzima ndoto bali ndoto inaweza kuvunja nguvu za shimo maana ndoto inatoka kwa mungu na shimo ni la wanadamu hivyo kwa kuwa ndoto yatoka kwa mungu basi ni lazima itakuwa na nguvu za mungu ndani yake ambazo hufanya kazi kwa wakati na wakati huo ukifika lazima shimo limtapike mwenye ndoto na ndoto hiyo huanza kutimia=habakuki 2:2-3.
Watu wengi wakitupwa kwenye shimo huwa wanafuta ndoto kwa sababu hawajui kuwa nguvu ya kuwatoa kwenye shimo ipo ndani ya ndoto hivyo wanafanya makosa makubwa sana nisikilize mwanangu shimo lisifute ndoto yako shimo la ugonjwa shimo la umasikini shimo la kutengwa shimo la utasa shimo lolote lile usikubali likufutie ndoto yako
Wakati flani miaka ya nyuma kidogo nalikuwa na ndoto yangu lakini baadae shetani akanitupa kwenye shimo ili nikate tamaa ya kutimia kwa ndoto yangu lakini mimi sikuifuta ndoto yangu ndani ya lile lile shimo mtoto wa kiume nikajikaza nikaendelea kuiweka ndoto yangu moyoni kamwe sikukubali ifutike. Baada ya muda marefu sana kupita nguvu ya ndoto yangu ikanitoa ndani ya lile shimo hata ndoto yangu ikatimia ooh jesus power ndiyo maana nasema shimo lisifute ndoto yako wakikutumbukiza kwenye shimo huku wanakuuliza unawaza nini wewe waambie nawaza kutumia kwa ndoto yangu

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni