YESU NI JIBU

Jumapili, 21 Februari 2016

KILA MMOJA ANA NJIA YA KUFIKA MAHALI AMA KUFIKIA MALENGO ILA YESU NI NJIA YA UZIMA NA MILELE BILA YEYE HUWEZI KUMWONA MUNGU.

Askofu Geofrey Masawe askofu wa jimbo la Mashariki Kasakazini na pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG Sahara Spiritual Center
 Mwinjisti Kambona Mwansasu Akifundisha somo la Njia ni Yesu katika kanisa la TAG sahara Spiritual Center.

 Waumini wakifuatilia neno kwa makini,
Imeelezwa kuwa njia peekee ya kufikia mafanikio na uzima wa milele ni kumkubali Bwana Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako kama mwanadamu maana nyakati za leo kuna matukio na njia nyingi.
Hayo yamesemwa na mwinjilisti Kambona mwansasu wakati akifundiso somo la Yesu ndiye njia ile katika kanisa la TAG Sahara Spiritual Center jijini Da es salaam.
Aidha mwinjilisti Mwansasu alisema kuwa kuna njia nyingi ambazo mwanadamu anaweza kutumia kufanikiwa na njia ni muhimu ili kufikia malengo ama jambo fulani,ila kupata na kufikia uzima wa milele ni Yesu pekee hakuna mwingine.
Alisema kuwa hapo awali katika bustani ya Edeni alikulaa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya na ndipo Mungu alimfukuza katika bustani na kuweka walinzi kulinda bustani,Akifafanua alisema kuwa lengo la malaika hao waliokuwa wakilinda bustani nia ni kulinda njia ya kurudi bustanini Adamu asije akala tunda la uzima wa milele.
Hapo njia ndiyo iliyofungwa na mpaka hapo Yesu alikuja na kuzaliwa kama mwanadamu kwa lengo la kumkomboa mwanadamu ili uwepo na ushirika kati ya Mungu na mwanadamu,jambo ambalo linawasaidia na kuwakomboa wanadamu katika madhaifu na magonjwa yao.
Akinukuu kitabu cha Yohana 14:6, 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 
7 Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. 
NA Yohana 5:24.

24 Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani. 
”Hakuna sababu ya kutumia njia zingine zaidi ya Yesu Pekee maana utakuwa na uhakika wa kufika kwake Baba wa Mbinguni,
Fanya bidii katika kumtafuta Yesu maana ndiye atakekuongoza kufika mbinguni ndiye njia sahihi wala wewe usikosoe wala lkuirekebisha.
Maana unakuta mwingine anaambiwa kuvuta sigara ni dhambi anaanza mjadala kuwa imeandikwa wapi? sasa pale utakapofahamu njia ya kweli kuwa ni Yesu hakuna sababu ya malumbano maan tayari unaifahamu njia."alisema mwinjilisti Mwansasu

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni