YESU NI JIBU

Ijumaa, 20 Desemba 2013

INJILI INAZIDI KUHUBIRIWA KILA KONA.

Yesu anazidi kuhubiriwa kuashiria kuwa ni nyakati za mwisho kwani kila kona injili imekuwa ikihubiriwa na watumishi mbalimbali katika mikutano ya hadhara ama nyumba kwa nyumba ama katika vituo vya daladala.
kutokana na hilo katika kanisa la Tanzania Assemblies of God TAG Gospel Campain limewasha moto wa injili katika viwanja vya kanisa hilo yalioko maeneo ya Majumba sita.
Katika Mkutano huu wa injili ishara na maajabu mbali mbali yametokea ambapo kunashuhuda mbalimbali ambazo zimetolewa katika viwanja hivyo vya kanisa hilo huku mtoto mmoja akielezea alivyopatwa na pepo la ulevi na mwingine kushuhudia alivyokuwa akishirikiana na wachawi na hao wote ni wanafunzi.Na cha kushangaza zaidi ni mwanamke ambaye amekuwa mgonjwa kwa muda wa miaka minne na kufikia kiwango cha kutoweza kutembea baada ya maombi akaanza kutembea kidogokidogo jambo ambalo limewavutia wengi ambao wamefika katika mkutano huo wa Injili pia kuwavutia wasikilizaji wa WAPO Redio waliokuwa wakisikiliza mkutano huu ukihubiriwa kupitia redio hiyo.
Mkutano huo ambao umeanza tarehe 8 desemba na itahitimika tarehe 29 desemba imeanza kuonesha mafanikio makubwa na ulifungua na mchungaji  Abdiel Mshashi kutoka Kilimanjaro na kupokelewa na mwenyeji Mchungaji Moses Maghembe na hatimaye kuhitimishwa na mchungaji Elia Lugwami.

Mchungaji Moses Maghembe akihubiri katika mkutano wa injili ulioanza kuanzia tarehe nane na inatarajiwa kuhitimishwa tarehe 26 desemba.Amekuwa akifundisha juu ya unabi kutimia.



Mmoja wa mtoto  akitoa ushuhuda wake



Huyu katikati anayeshikilia ni mwanamke ambaye amekuwa mgonjwakwa muda wa miaka minne bila kutembea mara baada ya maombi aliweza kutembea kidokidogo


 Hawa ni baadhi ya waumini waliofika katika mkutano wa Injili wakiwa makini kufuatilia mahubiri.





 Baadhi ya watu waliofika kwenye mkutano na wakati wa maombezi kujitokeza mbele kuongozwa sala na toba pamoja na kupata maombi na maombezi kutokana na matatizo mbalimbali

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni