YESU NI JIBU

Jumapili, 20 Oktoba 2013

HAIJAWAHI KUTOKEA VIJANA KUFURIKA KATIKA KONGAMANO LA VIJANA BCIC MBEZI BEACH

Kongamano la kuridhisha vipawa kwa vijana wa kizazi kipya limekuwa la tofauti pale ambapo walihudhuria vijana wengi zaidi ya elfu mbili.
Akizungumza wakati wa kufundisha somo la kuridhisha vipawa askofu Silyvester Gamanywa alisema kuwa ni vyema vijana wakaridhishwa vipawa ili tuwapate viongozi waadilifu na wanaomcha Mungu na ambao wataweza kubaba majukumu wakati waliopo  kwa sasa watakuwa hawapo katika ulimwengu.
Aidha askofu Gamanywa amewataka vijana kuacha lugha za malalamiko juu ya suala la kazi kuwa ni vyema kujituma na kujiajiri na kuacha malalamiko na kulaumu badala yake waanze kutafuta njia mbadala ya kuwakomboa kimaisha na kuepuka wimbi na lindi kubwa la ukosefu wa ajira.
 hata hivyo kjatika kongamano hilo walikuwepo walimu mbalimbali amabao walifundisha maada mbalimbali,ila mwalimu mkuu katika semina hiyo alikuwa askofu Gamanywa na mchungaji Peter Mitimingi ambaye kyeye alifundisha suala zima la mahusiano ambapo vijana wengi walionekana kufunguliwa katika somo hilo.
Wakati akifundisha mchungaji Mitimingi alisema kuwa kluna baadhi ya vijana ambao hawapendi kujishughulisha badala yake wamekuwa wapkipenndakupewa vitu mbalimbali, pia aliongeza kuwa ni vyema kuwepo kwa heshima na nidhamu ya hakli ya juu kati ya vijana wa kike na kiume.


 Askofu Slyvester Gamanywa akizungumza mara tu baada ya kongamano funguliwa rasmi.
 Askofu Gamanywa akimtambulisha mchungaji Peter mitimingi mwenye T shirt katika kongamano la vijana katika ukumbi wa BCIC Mbezi Beach jijini Dar es salaam
 Mchungaji Mitimingi mara baada ya kutambulisha alielezea jinsi alivyomfahamu askofu Gamanywa na kuelezea juu ya maono yake ya kuanzisha huduma ya Voice of Hope jinsi alivyomshirikisha na kutaka ushauri kutoka kwake.

Hapa anapokea nafasi kuendelea kutoa mafunzo kwa vijana walofika katika ukumbi huo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni