Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa BCIC Mbezi Beach jijini Dar es salaam ambapo walishiriki pia waalimu mbalimbali kutoa elimu na pia baadhi ya viongozi wa serikali nao walihudhuria katika kongamano hilo.
Vijana wengi waliohudhuria ni kuanzia miaka 12 hadi 35 na wengi wamekuwa na msisimuko mkubwa wa kutaka kufahamu hali halisi na jinsi ya kuweza kuridhi na zaidi ni kufahamu vipawa vyao katika jamii.
Kiukweli hili lilionesha jinsi vijana wengi walivyo na shauku ya kutaka kufahamu ni jinsi ganiwanaweza kuepukana na wimbi la umaskini na ukosefu wa kazi ama ajira.
Mwalimu Wilbroad Prosper akifundisha juu ya vipaji katika kongamano vijana ambalo limefanyika katika ukumbi wa BCIC Mbezi beach jijini Dar es salaam.
askofu Gamanywa akimtambulisha mwanaharakati Renatus Mkinga.
Mr Mkinga mara baada ya kutambulishwa na Askofu Gamanywa kwa vijana kwenye kongamano naye aliweza kuzugumza nao na kusema amefurahi kukutana na mwalimu wake wa chuo kikuu Profesa Bavu.
Mkurugenzi wa idara ya michezo vijana na utamaduni akizungumza kwenye kongamano.
Mwimbaji wa Rapu ndugu Rungu la Yesu ambaye anatamba na kibao cha YESU okoa mitaa akiwa anatumbuiza katika ukumbu wa BCIC
Hawa ni baadhi ya vijana waliohudhuria katika kongamano la vijana la kuridhisha vipawa na utajiri wakifuatilia kwa makini kongamano hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni