YESU NI JIBU

Jumapili, 22 Desemba 2013

KONGAMANO KUBWA LA SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGULIWA EAGT CITY CENTER

Kongamano kubwa na la siku 21 za maombi na maombezi ya kufunguliwa njia inaendelea katika ukumbi wa Ngoro ngoro katika viwanja vya maonesho vya mwalimu Julias Kambarage Nyerere maarufu kwa viwanja vya sabasaba.
Kongamalo hilo lilianza toka terehe 11 desemba na litahitimika tarehe moja januari mwaka 2014,kongamano hilo limeandaliwa na kanisa la EAGT City Center linaongozwa na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo mchungaji Florian Katunzi.
Katika kongamano hilo watu mbalimbali wameweza kufunguliwa matatizo yao mbalimbali ambapo kijana mmoja ameweza kushuhudia jinsi alivyofunguliwa na matatizo ya kuchanganyikiwa na kuwa kichaa ila bwana YESU alimfungua kupitia kwa mtumishi wake Mch Katunzi katika kongamano hilo ikiwa ni siku ya kuni na moja.
Waimbaji mbalimbali wanamtukuza MUNGU kwa njia ya uimbaji katika kongamano hilo ikiashiria siku ya mwisho wa kongamano hilo ambalo litahitimishwa kwa tamasha kubwa la kufungua mwaka tarehe moja januari mwaka 2014 katika ukumbi wa P.T.A kuanzia saa nane mchana.
Mchungaji Florian Katunzi akifundisha katika kongamano ;a maombi na maombezi katika ukumbi wa ngorongoro.
Huyu ndiye kijana ambaye aliletwa kwenye konamano akiwa amechanganyikiwa akishuhudia alivyofunguliwa na Bwana YESU.


hapa dada yake akishuhudia jinsi walivyokuwa wanamhudumia kiasi kwamba alikuja mganga na kusema yeye ni nabii anaweza kumsaidia bado hakukuwa na mafanikio.

Mwimbaji Emanuel Doboko akiwajibika katika madhabau ya EAGT kwenye ukumbi wa Ngorongoro


 Anafuata ni mwimbaji Atosha Kissava ambaye pia alikuwa ni mmoja wa waimbaji waliohudumu katika kongamano hilo na wanaendelea kuhudumu hadi siku ya kongamano.





 Huyu ni Stela Joel akiimba katika kongamano kubwa la maombi na maombezi.
 Mwimbaji Mess Chengula ndani ya ukumbi wa Ngoro ngoro


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni