YESU NI JIBU

Jumapili, 29 Desemba 2013

MAOMBI NA MAOMBEZI YANAENDELEA NDANI YA UKUMBI WA PTA KUFUNGULIWA KATIKA VIFUNGO MBALIMBALI

Hivi ndivyo ilivyo katika ukumbi wa PTA mara baada ya mchungaji Katunzi kuanza kuombea watu wanaopita katika mapito magumu na wengine waliweza kufunguliwa katika vifungo vya giza.
Ni jambo la busara sana kuamua kuchagua fungu jema badala ya kuchagua fungu lilobaya tena la mateso sana.
Akizungumza na blog hii mchungaji Katunzi alisema kuwa matokeo ya maombezi na maombi ya siku 21 imeonesha njia sana kiasi kwamba watu wengi waliofika kupata maombi ya uponyaji wa kazi,familia zao wameelezea jinsi walivyofunguliwa katika maombi hayo.
Aidha mchungaji alisema kuwa kwa sasa ni kuwaombea wanandoa ambao ndoa zao hazina amani wana furaha kuna mafarakano sambamba na kuwaombea mabinti ambao hawajaolewa ili wawapate wenza wa maisha wanatoka kwa MUNGU. 
Hivi ndivyo mapambano ilivyokuwa ikiendelea katika ukumbi wa PTA ambapo watu wengi wamefunguliwa 


Watu waliokuwa wakibebwa tayari kwa maombezi katika ukumbi wa PTA










Mchungaji Katunzi akiwaombea watu waliokuwa wakisumbuliwa na matatizo  mbalimbali 

Hivyo ndiyo hali ilivyo ni kuinua mikono juu kuashiria huwezi ama umesarender

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni