YESU NI JIBU

Jumamosi, 28 Desemba 2013

MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA NDOA YA ASKOFU DR MWENISONGOLE WA TAG (UPANGA CHRISTIAN CITY CENTER )

Imekuwa ni wakati wa nderemo na shangwe kwa familia na kanisa la askofu na mchungaji kiongozi wa kanisa la Tanzania assemblies of God Upanga Christian City Center Askofu Dr Renwell Mwenisongole kuadhimisha mika 40 ya ndoa yake.
askofu Mwenisingole aliwahi kuwa askofu mkuu wa TAG  na kwa sasa amestaafu na kuwa mchungaji wa kanisa la mahali pamoja UCCC.
Wakati akihubiri katika ibada hiyo ya kuadhimisha mika hiyo 40 askofu alisema anamshukuru Mungu maana amekuwa kimbilio na msaada wa maisha yake na kiukweli alimponya mara nyingi na amepitia na kupata ajali mara nyingi kiasi ambacho mke wake alivunjika mguu na bado haujapona vizuri mpaka sasa. ila anamshukuru Mungu kwa kumponya na hayo yote mpaka sasa anadhimisha miaka 40.
Naye mkurugenzi wa wanawake wa kanisa hilo WWK na pia ni mbunge wa viti maalum mhe.Rebeka Mgodo alisema kuwa ni jambo la furaha sana kusherekea miaka 40 ya ndoa na askofu Mwenisongole na ni mfano wa kuigwa na washirika wa kanisa hilo na watu wengine wanamfahamu mchungaji huyo kwa hiyo ni jambo jema sana.
Askofu Dr Mwenisongole na mkewe wakikata keki kwa pamoja tayari kulishana na kuwalisha  watu wengine.


Askofu akilishana keki na mkewe na sehemu nyinine na mzee walioanza huduma kwa pamoja.


Mheshimiwa mbunge na mkurugenzi wa WWK Mgodo akizungumzia maadhimisho hayo ya miaka 40  ya ndoa ya askofu Dr Mwenisongole na kuwapa mkono wa pongezi kwa niamba ya wanawake wa kanisa hilo waliotoa zawadi ambayo haipo pichani




Picha za matukio mbalimbali ya askofu Dr mwenisongole na mkewe pamoja na waumini.
Mchungaji Eliud Eseko ambaye ni mchungaji msaidizi katika kanisa hilo la UCCC.


Mch,Dr Esseko akiwa na mke wake kanisani

Mchungaji Esseko kulia akifurahia jambo analoambiwa na mkwe huku mke wa mchungaji Emanuel naye akicheka kwa furaha kwenye maadhimisho ya 40 ya ndoa ya askofu.






 Hivi ndivyo ilivyokuwa kanisa la UCCC.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni