YESU NI JIBU

Jumatano, 31 Mei 2017

WALIOFUNGWA NA KUKATA TAMAA SASA WAFURAHIA UPONYAJI NA UKUU WA MUNGU KATIKA MAISHA YAO BAADA YA KUPOKEA MIUJIZA YAO.

 baadhi ya waumini waliohudhuria kongamano wakimshika Mtumishi wa Mungu mchungaji Florian Katunzi kabla ya maombi na maombezi wakati wakihitimisha kufundisha neno la Mungu hali ambayo ilikuwa tofauti sana,

 Bi Sofia Abrahamu akliombewa na mchungaji Katunzi jumapili iliyopita baada ya kufika madhabahuni kutoa sadaka ya shukrani na kutengua mafungo na nguvu za mizimu ambayo imekuwa ikimwandama
 Bibi ambaye hakufahamika jina lake mara moja akishuhudia jinsi Mungu alivyomponya wakati aliteseka kwa muda mrefu bila mafanikio ila baada ya maombezi Mungu alimponya nasasa ni mzima anatembea bila Gongo.


Bibi ambaye hakufahamika jina lake mara moja akiwa na mchungaji Katunzi ambaye alikuwa na shida kwenye mguu hali iyopelekea kutafuta msaada katika njia mbalimbali na kulekea kuambiwa afanyiwe upasuaji iliyogharimu milioni 9 na Baada ya maombi na maombezi alianza kutembea hali iyopelekea kumtukuza Mungu na kutembea bila kushika tena gongo ambapo hapo awali alikuwa hawezi.
 Waumini waliofika kanisani hapo EAGT City Center wakifuatilia neno kwa makini ambalo mtumishi wa Mungu mchungaji Katunzi alifunzisha hayupo pichani.
 mchungaji Florian Katunzi Akiwaombea waumini waliofika madhabahuni kuombewa wakati wa kuhitimisha kongamano la maombi la siku tatu ndani ya kanisa la EAGT City Centter wiki iliyopita
 Mchungaji Katunzi akionesha fimbo ya kutembelea ambaye alikuwa akitumia mwanamke aliyefika kanisani hapo kutafuta maombi na maombezi na baada ya maombezi alitembea huku washirika wakishangilia matendo mak
 Mwanamke ambaye amefahamika kwa jina la SOfia Abraham akishuhudia matendo makuu ambayo Mungu amemtendea ndani ya kanisa la EAGT City center
  Wahudumu wakiwasaidia watu waliodondoka wakati wa maombi na maombezi kwa watu waliofungwa na nguvu za giza mizimu ya ukoo na shida mbalimbali.
Kongamano la siku tatu ndani ya kanisa la eagt city center limekuwa msaada kubwa kwa baadhi ya watu ambao walikuwa wanteseka kwa muda mrefu ssan katika maisha ya o hali iliyopelekea kushindwa kustawishwa katika maisha yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watu mbalimbali waliofika katika kanisa la EAGT City Center waliokuwa na matatizo mbalimbali wasimulia walivyokutana na Jemedari Yesu na kuwafunguwa na kuwaweka huru katika maisha yao.
Mwanamke ambaye amefahamika kwa jina la bi sofia abrahamu mwasumbi  alisema kuwa kupitia kongamano la siku tatu la maombi alisema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akiteseka katika maisha yake.
Akizungumza mbele ya kanisa hilo alisemea kuwa kwa muda mrefu amekuwa akipoteza fedha na kutesemka katika maisha yake kila anachokifanya hakifanikiwi n a amekuwa akipoteza fedha kwa muda mrefu hali ambayo imesababisha maisha yake kushindwa kufanikiwa .
“Nimeteseka sana katika maisha yangu maana katika familia yetu watnafamilia huwa akifa anafariki kutokana na ugonywa wa kuapararalize kupooza,ugonjwa ambayo inawattesa familia na kwa sasa name ninapata gansi upande wa kushoto”,alisema bibi Sofia.
Kutokana na hilo niliamua kujiunga na kanisa la EAGT CITY CENTER ambapo kulikuwa kuna maombi ya ukombozi na kufunguliwa yaliyokuwa yakiongozwa na mchungaji Florian Josephat Katunzi na Mungu alinitendea muujiza nimefunguliwa na kuwekwa huru kwa sasa ni jambo la kumshukuru sana Mungu.
“Tangu nianze kuwa mshirika wa kanisa hili Mungu amenitendea mambo makuu sana nimepona na ninaendelea vizuri nimetengwa na mateso na magonjwa ya kila namna na ninasimama kwa sasa mbele za Mungu na madhabahu kutangaza ushindi wa Mungu katika maisha yangu”alisema Sofia
Akiwaongoza katika maombi na maombezi  mchungaji Katunzi alinukuu kitabu cha Zaburi 107:13-14 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. Aliwatoa katika giza na uvuli wa mauti, Akayavunja mafungo yao.ni wakati wako Mungu kukutoa katika mateso na taabu za kila namna maana yeye ndiye kimbilio la wote wenye miili.
Mchungaji Katunzi aliongeza kuwa inawezekana umeteseka kwa muda nrefu kiasi kwamba umekata tamaana kuona kuwa haiwezekani tena kama biblia inavyosema kuwa akawaponya na shida zao leo Mungu kwa jina la Yesu Krisyto anaachilia nguvu ya uponyaji na uzima  juu ya kila mmoja aliyeingia ndani ya kanisa hilo.
Aliongeza kuwa Mungu anamponya mtu ambaye amejitenga na uovu na kusimama katika zamu yake na kuishi maisha ya utakatifu pamoja na kuliitia jina la Yesu Ili ufunguliwe katika mateso mbalimbali na magonjwa  sawa na kitabu cha zaburi 103:3-5 inayosema kuwa Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai; 
Ni kwanini unakubali kuteseka na kudanganywa na waganga wa kienyeji wakati Yesu mtenda miujiza Yupo kukuponya na mateso na magonjwa mbalimbali yanayokusibu katika maisha yako inawezekana hakuna kufanikiwa ndani ya familia,ukoo ana jamaa yako kutokana na mateso na vifungo mbalimbali mliofungwa ni wakati wa kukataa na kusima katika zamu yako ili bwana Yesu akufungue.
Kutokana na hilo mchungaji Katunzi ameendelea kutoa mwaliko kwa wale wote wanaoonewa na kuteseka kutokana na nguvu za giza,mizimu mafungo ya kila namna ili Mungu awafungue maana yeye Yupo tayari kuwasaidia wanadamu na kuwaweka huru katika maisha yao ya kielimu,kiuchumi na kiafnya.
Ndugu msomaji fuatilia mafundisho ya mchungaji Florian Katunzi kipindi cha saa ya ushindi na kufunguliwa kinachorushwa na Star TV kila siku ya jumamosi  saa moja hadi saa mbili usiku na marudio ni alhamisi saa nne na nusu hadi saa tano na nusu asubuhi.
Kwa mawasiliano piga simu namba 0718261717,0784367826 au 0754367826
Au tembelea www,pastorkatunzi.blogspot.com

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni