YESU NI JIBU

Jumatano, 2 Agosti 2017

USHAURI KWA WAZAZI JUU YA WATOTO WAO WANAOSOMA SHULE ZA KULALA.

Wazazi wanatakiwa kuwa makini na watoto wao hasa wale ambao wanapenda kuwapeleka watoto shule za kulala (boarding)iwe ya wasichana wenyewe  ama ya wavulana wenyewe,ni vizuri kuwa makini na kuhakikisha kuwa kila unapompeleka shuleni akirudi hakikisha kuwa unamsikiliza na kukaa naye ili ufahamu kuwa amekutana na changamoto gani akiwa huko shuleni.
Wazazi wenzangu nimekaa na kutafakari sana juu ya watoto wanaopelekwa shule za kulala watoto maana hali ni mbaya katika shule hizo maarufu kama (boarding).

Unaweza kulauliza ni kwanini nasema hivyo je sipendi watoto wasome shule za (boarding) hapana napenda tena sana ila sasa kilanachotokea ni kwamba watoto hao wanakutana na changamoto mbalimbali na wanajifunza na kuiga tabia ambazo ni mbaya na zinapelekea hata kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao.
Watoto wengi wanaosoma katika shule za kulala hasa wasichana pekee yao wanafundishana kufanya mapenzi ya jinsia moja sasa mtoto anarudi likizo hata mzazi hana muda wa kukaa naye wala kuzungumza naye mpaka tena shule inafunguliwa anarudi mzazi,mlezi hujafahamu changamoton na yale yanayomsimu mtoto.
Kwa upande wa shule za kulala watoto wa kiume nayo changamoto ipo kama ya wasichana  nao wanafanya na kufundishana mapenzi ya jinsia moja(ushoga) unakutana na kijana mtaani anajihusisha na masuala hayo unaanza kujiuliza umeanza lini,wapi? kumbe mzazi wewe ndiye uliyefungua mlango.
Unaweza kusema kuwa mimi mwanangu anasoma shule inayoendeshwa kwa misingi ya dini,swali Je unauhakika kuwa mwanao anajifunza dini ama anasikiliza wakati wewe hujamfundisha na hujawahi kuzungumza naye? ni swala la kujiuliza na kuwa makini nayo la sivyo utakuwa unaandaa kizazi kitakachokuwa shida.
Mzazi inakupasa kuwa makini na watoto ambao Mungu amekupa uwalinde uwasaidie wamjue na kumtambua Mungu wa kweli katika maisha yao,maana inakuwaje mzazi mwanao anarudi kutoka shuleni hata siku moja hujawaki wakupa muda wa kuzungumz anaye mapaka anarudi shuleni,
kibaya zaidi mzazi unakuwa nyumbani mwanao wa kiume anamleta rafiki wake wa kike anakaanaye nymbani kwako chumba kimoja baba mama hujui hilo si tayari ni tatizo halafu unasema kuwa wewe ni mzazi ama mlezi utakuwa unamatatizo hapo ghorofani (nikiwa na maana kichwani mwako)huwezi kuwa baba mama ama mlezi kwa namna hiyo wewe ni bora mzazi na sio mzazi bora,narudia wewe ni bora mzazi na sio mzazi bora.
Pamoja na maisha kuwa magumu na kukimbizana kila kukicha ni vyema ukatenga muda wa kuzungumza na watoto wako hata kwa dakika tano tafakari  maana ndiyo sababu  Mungu kakuamini na kukupa nafasi hiyo ya kuwa baba,mama au mlezi.
Watoto wengi wanapokuwepo mashuleni hujifunza mambo mengi ambayo hata mzazi unaweza kushangaa na kuchanganyikiwa usimuliwa yale mwanao anafanya,wengine wanafundishwa uchawi na ushirikina,usagaji,ushoga,wizi,ujambazi,matumizi ya madawa ya kulevya na mengine mengi yafananayo na hayo,mzazi upo wapi?
Kiukweli mimi binafsi inaniumiza kuona mzazi huna nafasi ya kukaa na watoto wako eti unadai wewe ni mkurugenzi,mhandisi,mchungaji,askofu,shekhe,Imamu na hata vyeo vyote ambavyo wewe unaweza kujiita,familia yako(watoto)ni wa muhimu kwanza kuliko hayo mengine.
Leo niishie hapa ila tujifunze kukaa na kuzungumza na watoto wetu waonyeshe upendo wa dhati na usiwanyime fimbo kama biblia inavyosema katika kitabu mithali 23:13-14 ambapo imeandikwa kuwa Usimnyime mtoto wako mapigo;Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.Utampiga kwa fimbo,na kumwokoa nafsi yake na kuzimu.

Kwa maswali ama jambo lolote nisms ama piga 0625620902 au 0779632616

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni