YESU NI JIBU

Jumatano, 2 Agosti 2017

WAWAUMINI WASHAURIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO ILI KUJIKWAMUA NA UMASKINI:

ASKOFU wa kanda ya kati kanisa la Pentecostal Holliness Association Mission (PHAM) Julias Bundala amewataka waumini wa  madhehebu ya dini kuhakikisha kuwa wanatumia fursa zinazojitokeza kwa wakati huu ambapo serikali imeamua kuhamishia makao yake makuu mkoani Dodoma.

Kiongozi huyo wa kanisa hilo ametoa ushauri huo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi mbalimbali wakiwemo wachungaji,wainjilisti,wazee wa kanisa na mashemasi kwenye semina ya siku nne iliyoandaliwa na kanda ya kati iliyofanyika kijiji cha Chiwe wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.


Amesema kuwa kutokana na uamuzi wa serikali kuhamishia makao yake ya nchi mkoni humo ni wakati sasa kwa waumini kuelekeza nguvu zao kwenye fursa zinzojitokeza ili waweze kujiinua kimapato na kuondokana na umasikini.


Akizungumza kwa upande wa viongozi wa kanisa hilo wakiwemo  wachungaji,wainjilisti,wazee wa kanisa na mashemasi,aliwataka  kuwa na ubunifu wa miradi itakayowaongezea kipato ili waweze kuondokana na changamoto walizonazo  kwenye maisha yao ya kila siku ikiwemo ya kiroho na kimwili.

Aliwataka viongozi hao walioshiriki katika semina hiyo iliyowashirikisha kutoka makanisa ya kanda hiyo ya kati ,askofu huyo amewataka kuwa na maono ya ubunifu katika utumishi wao yatakayowasaidia kuleta mapato ya kiuchumi kwa ajili ya maisha yao na jamii inayowazunguka.a kila siku.

Amesema na ili waweze kukamilisha katika utumishi wao huo wanatakiwa kuwa  vielelezo katika nafasi zao kwa uwajibikaji kwa kuonyesha matendo yao kwa uwazi  ili wanaowatumikia wawezi kujifunza kutoka kwao.

Pia askofu huyo alilitaka kanisa hilo kuhakikisha wanatumia muda wao mwingi kuiombeaserikali pamoja na viongozi wa nfgazi mbalimbali ili waweze kuifanya kazi zao kwa ueledi na hofu ya kimungu.

Aidha katika maombi hayo pia amewataka viongozi hao kuelekeze kwenye kumwaombea rais  aweze kutimiza yale yote ambayo yaliyo kuwa magumu kutekelezeka  katika vipindi vilivyopita vya viongozi waliomtangulia  ili afanikishe ndani ya uongozi wake wa awamu ya tano.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni