YESU NI JIBU

Jumatano, 29 Novemba 2017

SOMO:PONYA VIDONDA VYA MCHUNGAJI WAKO.

Luka 16:19-31" akasema,palikuwa na mtu mmoja,tajiri,aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi,na kula siku zote kwa anasa.na maskini mmoja jina lake lazaro,huwekwa mlangoni pake,ana vidonda vingi,naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka ktk meza ya yule tajiri;hata mbwa wakaja wakamlamba vidonda vyake.
Ikawa yule maskini alikufa,akachukuliwa mpaka kifuani kwa ibrahimu.yule tajiri naye akafa akazikwa.basi,kule kuzimu akayai ua macho yake,alipokuwa ktk mateso,akamwona ibrahim kwa mbali,na lazaro kifuani mwake.akalia,akasema,ee baba ibrahimu,nihurumie,umtume lazaro achovye ncha ya kidole chake majini,auburudishe ulimi wangu;kwa sababu ninateswa ktk moto huu.

Ibrahimu,akasema,mwanangu,kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea  mambo mema yako ktk maisha yako na lazaro vivyo alipata mabaya;na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa,na wewe unaumizwa.na zaidi ya hayo,kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze;wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.akasema,basi baba nakuomba umtume kwenda nyumbani kwa baba yangu,kwa kuwa ninao ndugu watano,ili awashuhudie,wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.ibrahimu akasema,wanao musa na manabii;na wawasikilize wao.akasema,la,baba ibrahimu,lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu,watatubu.akamwambia,wasipowasikia musa na manabii,hawatawashawishwa hat mtu akifufuka ktk wafu"
habari hii inamtaja tajiri na lazaro,Tajiri ni muumini ndani ya kanisa.
luka 16:22-25kawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. 
tajiri anamuita ibrahimu baba,hivyo ni muamini sawa na kitabu cha wagalatia 3:7" fahamu basi,ya kuwa wale walio wa imani,hao ndio wana wa ibrahimu "
MUNGU anakuona wewe ni tajiri.
ufunuo 2:9" naijua dhiki yako na umaskini wako,(lakini u tajiri)najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni wayahudi,na sio,bali ni sinagogi la shetani"
*biblia inasema yule tajiri alikila kwa anasa.
*kula neno la mungu pasipo kutumika hiyo ni anasa.
"kufutahia tu mahubiri pasipo kuyatendea kazi ni anasa.
*kupoteza wakati na kuwa na udhuru mwingi ni anasa.
*kutojitoa kwa ajili ya bwana ni anasa.
##tunapaswa kujichunguza##
*lazaro ni mchungaji.
*amewekwa mlangoni ili akuchunge uwe salama.
*yohana 10:9" mimi ndimi mlango,mtu akiingia kwa mimi,ataokoka,ataingia na kutoka,naye atapata malisho"
*mchungaji huutoa uhai wake kwa ajili yako.
*yohana 10:11" mimi ndimi mchungaji mwema.mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo"
*adui ajapo kukushambulia wewe kwanza humuanza mchungaji ili usiwe salama.
*marko 14:27" yesu akawaambia mtakunguwazwa ninyi nyote kwa ajili yangu usiku huu;kwa kuwa imeandikwa,nitampiga mchungaji na kondoo watatawanyika"
*bw.yesu alisema wazi kuwa kanuni ya adui ni kimshambulia mchungaji kwanza ndipo amfikie kondoo.
*tajiri(muumini)alimlisha lazaro (mchungaji) makombo.
**je!mchungaji wako anakula makombo?
**yohana 4:34"yesu akawaambia,chakula changu ndicho hiki,niyatende mapenzi yake aliyenipeleka,nikaimalize kazi yake"
**mchungaji anahitaji kazi ya mungu isonge mbele.ndiyo chakula chake.
*pasipo kazi ya mungu kusonga mbele hupata vidonda.
"ponya vidonda vyake visije kulambwa na mbwa.
*vidonda vya mchungaji hupona pale aonapo ujenzi ndani ya kanisa unakamilika.
*vidonda hupona mchungaji aonapo watu wanaokoka.
*vidonda vya mchungaji hupona aonapo watu wanaongezeka kiidadi kanisani na wanakua kiroho.
**nini unafanya kwa ajili ya mchungaji wako?unamlisha makombo?

*unapoponya vidonda vya mchungaji wako utajihakikishia usalama wako na uzao wako.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni