1. Kwa
nini mfalme suleimani alipewa adhabu na Mungu wakati alianza vizuri naye kama
mfalme wa Israeli?
Answer: kwa
sababu ya kuabudu miungu ama kufuata miungu.
1wafalme 11:4(kukengeuka)mfalme alioa
wanawake waliokuwa wanaabudu miungu mingi (1wafalme 11:5-8)
2. Musa
alikuwa mlimani na Mungu kwa muda usiopungua siku 80 ama miezi miwili na siku
ishirini alikuwa akifanya nini
Answer:alikuwa
akiandika amri kuu kumi za Mungu.
3. kutokana
na hilo ni nini kilichosababisha kukaa muda huu wote huko mlimani?
Answer:Ni
kwa sababu awamu ya kwanza wana wa israeli waliasi na kuanza kuabudu sanamu ya
ndama walioitengeneza na kusema ndiyo Mungu wao ndipo musa aliposhuka kutoka
mlimani akavunja zile mbao mbili alizoandika amri,(kumbukumbu
la torati 9:16,18)
Awamu ya pili siku zingine 40 Mungu
alipomwita tena musa mlimani kwenda kumkabidi tena mbao mbili za mawe mfano wa
zile za kwanza(kutoka 34:4)
4. Kwa
muda wa miaka mitatu na nusu ambapo mvua haikunyesha juu ya nchi kwa neno la nabii
Eliya yeye akiwa nabii alikuwa analishwa na nani? kwa muda huo wote.
Answer:kwa
muda huo alijikuta akilishwa na kunguru na baadaye na mwanamke mjane wa sarepta(1wafalme 17:1-16)
5. Neno
Familia kwa mtazamo wa kibiblia lina maana gani?Toa Sababu kama ama maana tano.
Answer:
· Mume
na mke waliooana hata kama hawana watoto.
· Watu
wa familia moja lakini vizazi tofauti tofauti.
· watu
wanaokaa nyumba moja hata kama ni kutoka ukoo tofauti tofauti(kutoka 12:3)
· Watu
waliofunga maagano ya kushirikiana kwa karibu;kama vile
biashara,ndoa,mikopo,ardhi,utaifa,ndiyo maaana biblia inasema usifungiwe nira
na wasioamini 2kor 6:14)
· Watu
wa kabila moja kama vile watoto 12 wa Yakobo walipofanyika vyanzo vya kabila 12
za Israeli(mwanzo 49:1,2,28).
SHIRIKI KUJIFUNZA BIBLIA NA KAMA UNAMONI TOA KWA NAMBA 0779632616 AU 0682672828.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni