YESU NI JIBU

Ijumaa, 14 Novemba 2014

WAUMINI WA MCHUNGAJI FRANK KABELE WA HUKO NCHINI NIGERIA WAACHWA NA MASIKITIKO MAKUBWA BAADA YA MCHUNGAJI HUYO KUSOMBWA NA MAJI NA KUFARIKI DUNIA

Mchungaji Frank Kabele akiomba msaada ya kuokolewa bila mafanikio.
Ilikuwa sikitisho kubwa kwa waumini baada ya mchungaji wao kusombwa na maji baada ya kujaribu kutembea juu ya maji kama vile masihi Yesu alivyofanya wakati wake alipokuwa duniani ,hayo yametokea huko nchini Nigeria.
Pastor Frank Kabele mwenye umri wa miaka 35, aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani. Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake.

Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya pastor huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi.

Mfuasi wa Yesu, Peter alijaribu kutembea juu ya maji kama vile Yesu alivyofanya lakini hakutoboa, alisaidiwa kuzama maji. Sasa miaka zaidi ya 2000 baadae, pastor huyu wa Nigeria alijaribu kumuiga Yesu lakini hakufaulu na majibu yake ni kuwa alipoteza maisha yake.

Ama pastor huyo aliingiwa na imani kuwa anaweza kutembea juu ya maji kama vile wale 'magician' wa vipindi vya runinga wanavyofanya.

 Kiganja cha mchungaji akizama majini.
TOA MAONI YAKO NDUGU MSOMAJI.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni