YESU NI JIBU

Ijumaa, 14 Novemba 2014

KIONGOZI NA MMWASISI WA HUDUMA YA SILOAM AMEFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 54:

Kila huduma mara nyingi inapoanzishwa huwa inawekwa chini ya msingi fulani iwe mizuri ama la,iwe ya kumpendeza Mungu au sio  ya kumpendeza na waasisi wake huwa ndio wenye maono na ndoto za kuanzisha huduma hizo.
Hivyo mpendwa msomaji wa blog hii ni kazi kwako wewe kufanya chaguo jema la kuamua na kufanya maamuzi sahihi katika maisha yako ya kiroho.

                           Huyu ndiye nabii Eliya
Kuna habari zimeenea kwa kasi katika mitando ya kijamii ya kwamba ,mwenye mafundisho tata ,Ndugu Munuo,aka Adamu wa Pili, Nabii Eliya, Bwana wa Majeshi, Mjumbe wa Mapenzi ya Mungu wa Kizazi cha Nne, Amefariki Dunia, Akithibitisha juu ya tukio hilo la kifo cha nabii huyo,mratibu wa habari wa huduma hiyo ya Siloam International Bi Hakikazi Eliya ambaye jina lake la mwanzo ni Scolastica Msewa amesema kuwa amefariki na hakutaja chanzo cha kifo chake.
Aliyekuwa Nabii Eliya wa kanisa la siloam shika neno tenda neno akifundisha.
 Wafuasi wakijipanga wakati wa yeye kuingia.
Aidha msemaji alisema huyo alisema kuwa atazikwa au kuhifadhiwa nyumbani kwake Mapinga Bagamoyo mkoani Pwani (Mlima wa neno la Maono)ambapo mazishi yake yataongozwa na msaidizi wake wa karibu kuhani kiongozi ,miaka 1000 Eliya na mavazi yatakayovaaliwa nimeupe sio meusi kwa sababu kwao sio msiba ni sherehe hivyo kila kitu kitakuwa cheupe.
Nabii Eliya Mnuo (Eliya Adamu wa pili Mungu wa majeshi)amefariki akiwa na umri wa miaka 54 na kumwacha mke mmoja ambaye anafahamika kwa jina la mama siku saba madhabahu ya eliya na watoto wanne na wajukuu watatu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni