Mchungaji Aidan Mabuka
Kauli hiyo imetolewa na mchungaji kiongozi wa kanisa la
eagt mlima wa faraja mchungaji Aidan Mabuka katika mahojiano maalum na wapo
redio katika mkutano wa injili ambao umeandaliwa na kanisa hilo lilopo yombo
kisiwani kata ya sandali wilaya ya temeke jijini ambapo amesema kuwa ni vyema
serikali ikaweka mikakati kabambe ya kuwanusuru vijana na kuwashirikisha
viongozi wa dini.
Aidha amesema kuwa ni wajibu wa serikali na viongozi wa
dini kuungana kwa pamoja kwa lengo la kuwasaidia na kuwanusuru vijana katika wimbi
la utumiaji na uuzaji wa madawa ambao kwa sasa umekamata kasi katika baadhi ya
mataifa na kuwapelekea vijana kuteseka na nguvu kazi ya taifa inapotea.
Mhungaji kiongozi Mabuka akiwa na mke wake na wazee wa kanisa.Mke wa mchungaji Mabuka akifanya maombi kabla ya mchungaji kusimama kuhubiri katika mkutano wa injili ambao unaendelea katika viwanja vya Yombo kisiwani kwa fundi umeme jijini Dar es salaam.
Waimbaji mbalimbali wakihudumu katika mkutano huo wa injili ambayo mchungaji Aidan Mabuka ndiye mhubiri ambapo watu wengi wamefunguliwa na kuwekwa huru na wengi wamepokea uponyaji.
Watu waliofika katika mkutano wa injili kusikiliza neno la Mungu.
"Ni vyema kuwa karibu na vijana ambao tayari
wamekata tamaa kwa lengo la kuwajenga upya kisaikolojia ili waweze kuwa na
matumaini tena maana wengi wameshaona kuwa haiwezekani tena na hiyo mdiyo njia
pekee kwa kuwaonesha upendo wa kristo nao wataweza kurudi,"alisema
mchungaji mabuka.
Serikali kuu na ya mitaa inabidi iweke mkakati maalum wa
kuwanusuru wananchi wake hasa vijana ambao wanateseke na kuwapelekea
kushawishika kujiingiza katika makundi ya kihalifu hivyo ni wajibu wa serikali
kubuni mbinu mbalimbali za kuwasaidia ikishirikisha viongozi mbalimbali wa
dini.
Pamoja na hayo mchungaji mabuga hakuwa nyuma kutoa wito
kwa viongozi wenzake wa dini kuacha kulumbana na kusemana vibaya badala yake ni
kusaidiana ,kushauriana na kuombeana kwani ili waweze kumudu kupigana na adui
ni sharti uwepo umoja na muungano ndipo wataweza kupambana na adui.
Watumishi wa mungu ni vyema kuungana kwa pamoja ili
kuwafikia vijana na jamii yetu inayotuzunguka ili wampokee yesu kama bwana na
mwokozi wa maisha yao na kuachana na makundi mbalimbali ambayo hayasaidii wala
haijengi mwili wa kristo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni