YESU NI JIBU

Jumatatu, 30 Aprili 2012

HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA LA GOSHEN MINISTRY INTERNATIONAL LILOPO CHANIKA JIJI DA ES SALAAM

Kanisa la Goshen Ministries International lilopo Chanika jiji Dar es saalam limeandaa harambe ya kuchangia ujenzi wa kanisa na huduma za kijamii kama vile shule na hospitali.

Akizungumza katika harambe ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo naibu mstahiki meya wa jiji la Dar es salaam Chaurembo Abdala amesema kuwa ni vyema serikali kushirikiana na viongozi wa dini ili kuweza kuleta maendeleo kwa jamii.

Aidha Ndugu Abdala aliongeza kuwa huduma inayotolewa na viongozi wa dini inafahamika hivyo ni vyema kila mtu kujitolea kuchangia huduma hizo.

Naye mchungaji wa kanisa hilo mchungaji Emanuel Chakoa akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ambaye ni naibu mstaiki meye ambaye amemwakilisha meya wa jiji la Dar es salaam amesema kuwa wanahitaji kiasi cha milioni 200 kwa lengo la kujenga kanisa la kisasa


                                   
                                                        

 Kutoka kushoto ni mchungaji Emanuel Chakoa akiwa na Naibu mstahiki meya wa jiji la Da es salaam




Mchungaji Emanuel Chakoa wa kanisa la Goshen Ministries Intenation akizungumza katika harambee ambayo imefanyika jiji Dar es salaam






Hakuna maoni :

Chapisha Maoni